

Lugha Nyingine
Namna gani reli ya SGR imeweza kuwa ateri ya kijani nchini Kenya?
NAIROBI – Kunapoanza kupambazuka kwenye savana ya Kenya, kundi la twiga lilikuwa likipita taratibu kwenye matao yenye urefu wa mita 7.5 kwenda juu ya daraja la reli ya SGR ya Nairobi-Malaba, ambayo kimahsusi yamejengwa kukidhi urefu wao.
Takriban umbali wa kilomita tatu kutoka hapo, kamera maalumu zinarekodi mama kifaru akimwongoza ndama wake kupita ushoroba wa wanyamapori uliopambwa kwa michoro ya kabila la Wamaasai.
Matukio hayo, yaliyoshuhudiwa na waandishi wa habari waliokuwa wakisafiri nchini Kenya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Uanuai wa Viumbe Mei 22, yanaonesha falsafa kuwa uhifadhi wa kiikolojia si kizuizi, bali ndiyo msingi halisi wa maendeleo.
Ikiwa ilijengwa na Kampuni ya China Road and Bridge Corporation (CRBC), Reli ya SGR ya Nairobi-Malaba ni sehemu muhimu ya Mradi wa Reli ya SGR wa Kenya.
Kwa mujibu wa Yu Fujia, meneja mkuu msaidizi wa CRBC nchini Kenya, reli hiyo ina vivuko vya ardhini 14 vya wanyamapori, makalavati 150 ya chini ya ardhi, pamoja na vidhibiti kelele vya njia za kuvuka kwa juu zenye urefu wa kilomita sita vikiwa na vizuizi vinavyopitisha mwanga, vikiunda shoroba za pande tatu kwa wanyama.
"Utalii wa wanyamapori unachochea sana uchumi wa Kenya. Tusingeweza kumudu kutatiza hilo. Wakati mpango wa awali wa njia ya reli ulipotishia kutenganisha njia ya uhamaji wa nyumbu, wahandisi walihamisha njia ya reli kwa kilomita 15 kuelekea kusini, wakiongeza madaraja tisa na asilimia 12 kwenye gharama, ili kulinda uhamaji wa wanyama zaidi ya milioni mbili" amesema Yu.
Mbinu hiyo ya CRBC inachanganya hekima ya kale ya China ya kiikolojia na teknolojia ya kisasa. Karibu na Hifadhi ya Taifa ya Tsavo, katika sehemu ya kusini-mashariki mwa Kenya, mifumo ya mtikisiko wa tahadhari hutoa mitetemo ya ardhini inayofanana na mitetemeko ya asili, kwa upole ikiongoza makundi ya tembo kuelekea mbali kutoka kwenye reli.
Makazi ya viboko yanalindwa kwa reli za kupunguza kelele ambazo zimeundwa kupitisha sauti viwango vya decibel 55 tu, kimya zaidi hata kuliko upepo wa savana.
Nguzo za madaraja ya maeneo ya ardhioevu mjini Mombasa zimewekewa miamba ya matumbawe ya kutengenezwa na binadamu, ambayo tangu wakati huo yamekuza mifumo ya kiikolojia inayostawi ya mikoko.
"Kila uamuzi ulitoa kipaumbele kwa uvurugaji mdogo," Yu amesisitiza.
"Si tu walijenga reli, bali walisuka mtandao wa usalama wa kiikolojia," amesema Erustus Kanga, mkuu wa shirika la Huduma kwa Wanyamapori la Kenya.
SGR ya Kenya inasimama kama mfano wa kuigwa unaotambuliwa na Umoja wa Mataifa wa miundombinu endelevu.
Katika mapatano haya yasiyowezekana kikawaida kati ya chuma na savana, funzo lenye kauli linajitokeza: ustaarabu unapojifunza kusikiliza ardhi, maendeleo hayawi tena nguvu ya uharibifu, bali uwiano na ustawishaji upya.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma