Rais Hichilema ahimiza umoja wa Afrika yote wakati Zambia ikiadhimisha Siku ya Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2025
Rais Hichilema ahimiza umoja wa Afrika yote wakati Zambia ikiadhimisha Siku ya Afrika
Wanajeshi wakishiriki katika shughuli ya ukumbusho wa Siku ya Afrika mjini Lusaka, Zambia, Mei 25, 2025. (Xinhua/Peng Lijun)

LUSAKA - Zambia imeadhimisha Siku ya Afrika jana Jumapili, huku Rais Hakainde Hichilema wa nchi hiyo akitoa wito wa kudhamiria tena kwa mshikamano wa Afrika yote akisema ni muhimu kwa Afrika kudhamiria tena kuwa na mshikamano na kujumuika pamoja kwa kufuata moyo wa Pan-Afrika.

"Ili kufikia lengo hili, lazima tunyamazishe bunduki na kuwekeza kwenye amani. Kukosekana kwa utulivu popote barani Afrika ni kukosekana kwa utulivu kila mahali barani humo. Afrika haiwezi kumudu kugawanywa kwa migogoro wakati ndoto ya umoja na ustawi iko ndani ya kufikiwa," amesema.

Hichilema ametoa wito kwa viongozi wa Afrika kuweka kipaumbele katika ukuaji jumuishi unakita mizizi katika hali wazi, usimamizi makini wa mambo ya fedha na bajeti na dhamira ya kuhakikisha maendeleo yanaleta ajira na fursa kwa Waafrika wote.

Amesema Zambia itaendelea kutetea amani, usalama na utulivu, vilevile diplomasia ya uchumi ili kuchochea biashara ya ndani ya Afrika na ushirikiano wa kimataifa.

Amesema Zambia itaendelea kutetea usanifu wa mfumo wa mambo ya fedha wa kimataifa wenye usawa zaidi ambao hautaweza kuzidisha hali isiyo na usawa katika historia, bali unawezesha Afrika kuamua njia yake yenyewe kuelekea maendeleo endelevu.

Siku ya Afrika, inayoadhimishwa kila mwaka Mei 25, inakumbuka kuanzishwa kwa Jumuiya ya Umoja wa Afrika mwaka 1963, ambayo kwa sasa inajulikana kwa jina la Umoja wa Afrika. Kukumbuka siku hiyo ni kwa ajili ya kusherehekea umoja, amani na anuwai ya utamaduni wa Afrika. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha