

Lugha Nyingine
Maonyesho ya kimataifa ya kilimo yafunguliwa Cote d’Ivoire huku China ikiwa nchi mgeni wa heshima (6)
ABIDJAN - Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Kilimo na Rasilimali Wanyama ya Abidjan, ambayo ni maonyesho makubwa ya kilimo katika eneo la Afrika Magharibi, yamefunguliwa mjini Abidjan, Cote d'Ivoire siku ya Ijumaa, huku China ikishiriki kama nchi mgeni wa heshima.
Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa maonyesho hayo, Waziri Mkuu wa Cote d'Ivoire Robert Beugre Mambe amesema China ni "bingwa wa kilimo duniani" na mshirika muhimu katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini humo.
Huku akisema kuwa nchi hiyo imepata maendeleo katika uzalishaji na mauzo ya nje, waziri mkuu huyo amesema kilimo cha Cote d’Ivoire bado kinakabiliwa na changamoto katika uanuwai wa mazao ya biashara, usindikaji wa mazao, pembejeo za uzalishaji za kiwango cha juu, utumiaji mashine mashambani, na kupambana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.
Katika hotuba yake, Zhang Xingwang, naibu waziri wa kilimo na mambo ya vijijini wa China, amesema Cote d'Ivoire ni mzalishaji mkuu wa kimataifa wa bidhaa za kilimo kama vile kakao, korosho na mpira wa asili, wakati China inajivunia soko kubwa na idadi kubwa ya watumiaji, akiongeza kuwa nchi hizo mbili zina matarajio mapana kwa ushirikiano katika teknolojia ya kilimo, usindikaji mazao ya kilimo na biashara.
Maonyesho hayo ya siku 10 yanatarajiwa kuvutia watembeleaji zaidi ya 500,000 na waonyeshaji bidhaa karibu 1,000 wakionyesha bidhaa na huduma kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Ulaya.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma