Rais Xi aihimiza China, Korea Kusini kuinua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati hadi ngazi ya juu zaidi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping kwenye mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Korea Kusini Lee Jae-myung Jumanne amesema kuwa China na Korea Kusini zinapaswa kuinua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wao wa kimkakati hadi kwenye ngazi ya juu zaidi, ili kutoa manufaa zaidi kwa watu wao na kuleta uhakika zaidi wa amani katika hali yenye mabadiliko na misukosuko ya kikanda na kimataifa.

Akitoa pongezi kwa mara nyingine tena kwa Lee kwa kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Korea Kusini, Rais Xi amesema China na Korea Kusini ni majirani wa karibu wasioweza kuhamishika.

Katika miaka 33 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, nchi hizo mbili zimevuka tofauti katika itikadi na mifumo ya jamii, na kufanya juhudi za kuhimiza mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, hivyo kuchangia mafanikio ya kila upande na kupata maendeleo kwa pamoja," amesema.

Rais Xi amesema uhusiano mzuri, tulivu na unaoendelezwa kwa kina zaidi kati ya China na Korea Kusini, unaendana na mwelekeo wa maendeleo ya zama hizi, unalingana na maslahi ya kimsingi ya watu wa pande hizo mbili, na pia unachangia amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa kikanda na kimataifa.

"China na Korea Kusini zinapaswa kushikilia nia ya awali ya kuanzishwa kwa uhusiano wao wa kidiplomasia, kushikilia ujirani mwema na urafiki, na kufuata lengo la kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja," Rais Xi amesema.

Amesema, pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano kwenye ngazi mbalimbali katika sekta mbalimbali ili kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati, kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na uratibu wa pande nyingi ili kwa pamoja kulinda ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria, na kuhakikisha minyororo ya viwanda na usambazaji bidhaa duniani na kikanda iliyo tulivu bila vizuizi.

Rais Lee, kwa upande wake, amesema anakubaliana na Rais Xi, akisisitiza mchangamano wa kijiografia, mawasiliano ya muda mrefu na wa karibu zaidi kati ya Korea Kusini na China katika sekta za uchumi, biashara na utmaaduni.

Huku akisifu mafanikio makubwa ya maendeleo ya China chini ya uongozi bora wa Rais Xi, Rais Lee amesema anaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano kati ya Korea Kusini na China, na anapenda kufanya juhudi pamoja na China katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wao wa ujirani mwema na urafiki, kuongeza hisia njema kati ya watu wa nchi hizo mbili na kupata matokeo zaidi katika ushirikiano wa pande mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha