

Lugha Nyingine
Rais Xi na mwenzake wa Jamhuri ya Kongo Sassou Nguesso watuma barua za pongezi kwa Mkutano wa Mawaziri Waratibu wa Matokeo ya FOCAC
Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso kwa nyakati tofauti leo Jumatano wametuma barua za pongezi kwa Mkutano wa Mawaziri wa Waratibu wa Utekelezaji wa Matokeo ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), wakieleza pongezi kwa kufanyika kwa mkutano huo.
Mkutano huo unafanyika mjini Changsha, mji mkuu wa Mkoa Hunan katikati mwa China.
Kwenye barua yake, Rais Xi Jinping amesema, katika kipindi cha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, limesukuma kikamilifu maendeleo yenye ustawi ya ushirikiano kati ya China na Afrika na kuwa kielelezo cha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa nchi za Kusini.
Amesema kuwa, inatarajiwa kuwa China na Afrika zitaendelea kuhimiza kithabiti utekelezaji wa matokeo ya mkutano huo, kupanga kwa makini maendeleo ya siku za baadaye ya jukwaa hilo, kufanya kazi pamoja kujenga jumuiya ya hali zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na kuchangia nguvu ya China na Afrika katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.
Katika barua yake ya pongezi, Rais Sassou Nguesso amesema ikiwa mwenyekiti mwenza wa Afrika wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, Jamhuri ya Kongo inapenda kufanya kazi na China na nchi zingine za Kusini ili kuimarisha ushirikiano chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kwa pamoja kujenga dunia ya ncha nyingi yenye kuachana na uamuzi wa upande mmoja na kujihami, na kuingia katika zama mpya ya utandawazi jumuishi.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma