China na Marekani zafanya mazungumzo ya kitaalamu na ya wazi

(CRI Online) Juni 11, 2025

(Picha/CRI)

(Picha/CRI)

Mwakilishi wa biashara ya kimataifa ya China ambaye pia ni naibu waziri wa biashara wa China Bw. Li Chenggang amesema Jumanne kuwa katika siku mbili zilizopita China na Marekani zimefanya mazungumzo ya kitaalamu, yenye mantiki, ya kina na ya wazi.

Bw. Li ametoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia mkutano wa kwanza kati ya China na Marekani kuhusu utaratibu wa mashauriano ya kiuchumi na kibiashara uliofanyika mjini London, Uingereza.

Amesema kuwa, pande hizo mbili zimekubaliana kimsingi utaratibu wa kutekeleza makubaliano kati ya wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa mazungumzo yao ya simu ya Juni 5, pamoja na yale yaliyoafikiwa katika mazungumzo ya Geneva.

Ameeleza kuwa, inatarajiwa kwamba maendeleo yaliyopatikana katika mkutano wa London yatachangia kuimarisha kuaminiana kati ya China na Marekani, na kuhimiza zaidi maendeleo thabiti na yenye afya ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha