

Lugha Nyingine
China yahimiza jumuiya ya kimataifa kuziunga mkono nchi za Afrika ya Kati kukabiliana na matishio ya usalama
Mwakilishi msaidizi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuziunga mkono nchi za eneo la Afrika ya Kati kukabiliana na matishio ya usalama na changamoto za kibinadamu.
Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Afrika ya Kati uliofanyika jana Jumanne, Balozi Sun amesema changamoto za usalama katika eneo hilo bado ni kubwa, na kwamba matukio ya kimabavu katika Bonde la Ziwa Chad yanaongezeka, huku mashambulizi ya kigaidi katika eneo hilo yakiongezeka, sambamba na athari za hali ya Sudan na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinazozidi kuenea zaidi na kusababisha ukosefu wa utulivu wa eneo hilo.
Amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuziunga mkono nchi za eneo hilo kuimarisha uwezo wao wa kupambana na ugaidi, kuongeza uungaji mkono katika ufadhili wa kifedha, mabadilishano ya taarifa na ujengaji uwezo, ili kujenga ulinzi thabiti wa usalama.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma