Onesho la mitindo ya mavazi ya watu wanene nchini Kenya lasema 'unene ni urembo'

(CRI Online) Juni 11, 2025

Wakiwa na mavazi ya Kiafrika ya batiki na nguo za jioni zinazobana, wanamitindo wa maumbo makubwa "plus-size" walipanda kwenye jukwaa la kuonesha mavazi mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya, katika hafla maalum iliyoandaliwa ili kusherehekea urembo wa wanawake wanene zaidi.

Mbele ya watazamaji zaidi ya 300 waliokuwa wakiwashangilia, wanamitindo hao, wengi wao wasio wa kulipwa, walitembea na kucheza kwenye jukwaa la kuonesha mavazi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Maonesho hayo ya mitindo yaliangazia masuala ya afya lakini pia yanalenga zaidi “kuthamini wanawake wenye maumbo makubwa yaliyochongoka” na “kusherehekea mwonekano wao kwa kuchanganya na mitindo kutokana na ugumu wa kupata nguo,” amesema Walcott, ambaye ni mwandaaji wa tukio hilo.

Walcott alianzisha onesho hilo ili kutoa heshima kwa mama yake na kumfanya "kujiona ni mrembo."

“Unaona jinsi nilivyo mnene, nilikuwa nikiuchukia sana mwili wangu, lakini amenitia moyo sana,” amesema mamake Walcott, Seline Aoko, akiwa ndani ya kibanda cha matunda mjini Kisumu ambako anafanya kazi. "Unene ni urembo!"ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha