

Lugha Nyingine
Naibu Waziri Mkuu wa China aitaka Marekani kutatua migogoro ya kibiashara na China kupitia mazungumzo na ushirikiano
LONDON - Marekani inapaswa kutatua migogoro ya kibiashara kati yake na China kupitia mazungumzo sawa na ushirikiano wa kunufaishana, He Lifeng Naibu Waziri Mkuu wa China amesema kwenye mkutano wa kwanza wa utaratibu wa mashauriano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani uliofanyika jijini London, Uingereza kuanzia Jumatatu hadi Jumanne.
"China inasisitiza tena kwamba Marekani inapaswa kuendana na China kwa vitendo, na kuonyesha udhati katika kutunza ahadi na juhudi madhubuti kutekeleza maafikiano, ili kwa pamoja kulinda matokeo yaliyopatikana kwa bidii ya mazungumzo," amesema He kwenye mkutano huo pamoja na ofisa anayeongoza upande wa Marekani Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent, Waziri wa Biashara wa Marekani Howard Lutnick na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Jamieson Greer.
Amesema kuwa, katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimefanya mazungumzo ya wazi na ya kina, na kwa mapana kubadilishana maoni kuhusu masuala ya kiuchumi na kibiashara yanayofuatiliwa na pande zote mbili.
Kwenye mkutano huo, pande hizo mbili zimefikia makubaliano juu ya kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili wakati wa mazungumzo yao ya simu Juni 5 na mfumokazi wa hatua za kuimarisha matokeo ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara ya mjini Geneva, na kupata maendeleo mapya katika kushughulikia masuala ya kiuchumi na kibiashara yanayofuatiliwa na kila upande.
Akiuelezea mkutano huo kuwa mashauriano muhimu yaliyofanyika chini ya mwongozo wa maafikiano ya kimkakati yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili Juni 5, He amesema msimamo wa China kuhusu masuala ya kiuchumi na biashara kati ya China na Marekani uko wazi na usioyumba.
Huku akiongeza kuwa kiini cha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani kiko katika kunufaishana, naibu waziri mkuu huyo amesema ushirikiano kati ya China na Marekani katika nyanja ya uchumi na biashara unanufaisha pande zote mbili, huku makabiliano yanadhuru pande zote mbili.
.
“Hakuna washindi katika vita vya kibiashara,” He amesema, akiongeza kuwa China haitaka mgogoro lakini haitatishwa na mgogoro.
Ameitaka Marekani kusuluhisha migogoro ya kibiashara na China kupitia mazungumzo sawa na ushirikiano wa kunufaishana, akiongeza kuwa ingawa China ina nia ya dhati katika kufanya mashauriano ya kiuchumi na kibiashara, pia ina kanuni zake.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma