EU, Hispania, Uingereza, Gibraltar zaafikiana juu ya makubaliano ya mpaka huria ya siku za baadaye

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2025

Picha iliyopigwa Mei 23, 2025 ikionyesha bendera za Umoja wa Ulaya kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Picha iliyopigwa Mei 23, 2025 ikionyesha bendera za Umoja wa Ulaya kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

BRUSSELS - Maafisa waandamizi kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Hispania na Uingereza, pamoja na wawakilishi wa Gibraltar, wamefikia makubaliano mjini Brussels jana Jumatano juu ya vipengele vikuu vya mkataba wa baadaye kati ya EU na Uingereza kuhusu Gibraltar, unaolenga kuondoa vizuizi vya mpakani na kuendeleza ustawi wa kikanda.

"Makubaliano hayo ya siku za baadaye ni bila kuathiri nafasi husika za kisheria za Hispania na Uingereza kuhusiana na mamlaka na umiliki wa mipaka," imesema taarifa ya pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, lengo la makubaliano hayo ya siku za baadaye ni kupata ustawi wa eneo hilo kwa kuondoa vizuizi vyote vya kimuundo, ukaguzi na udhibiti wa watu na bidhaa zinazozunguka kati ya Hispania na Gibraltar.

Hii itafanywa huku wakati huohuo ikihifadhi eneo la Schengen, soko pekee la Umoja wa Ulaya, na umoja wa forodha.

Watu wakitembea mtaani huko Gibraltar, Machi 30, 2021. (Picha na Pablo Morano/Xinhua)

Watu wakitembea mtaani huko Gibraltar, Machi 30, 2021. (Picha na Pablo Morano/Xinhua)

Kuhusu mzunguko wa watu, taarifa hiyo inaeleza kuwa ukaguzi mpakani kati ya Gibraltar na La Linea ya Hispania utaondolewa kwa watu wanaovuka kila siku kwenda kazini huku ukaguzi wa mara mbili utafanywa katika bandari ya Gibraltar na uwanja wa ndege.

Kuhusu bidhaa, taarifa hiyo imeeleza kuwa ushirikiano imara kati ya mamlaka za pande zote mbili za forodha na uondoaji ukaguzi kwenye bidhaa utahimiza kuunda umoja wa forodha kati ya EU na Gibraltar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, maeneo mengine yatakayohusiana na makubaliano hayo ya baadaye ni pamoja na misaada ya Serikali, kodi, kazi, mazingira, biashara na maendeleo endelevu, kupambana na utakatishaji fedha, usafiri, mshikamano na ajira.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha