

Lugha Nyingine
Biashara kati ya China na Afrika katika miezi 5 ya kwanza ya mwaka huu yavunja rekodi
BEIJING — Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mamlaka Kuu ya Forodha ya China ya Jumanne wiki hii, kiwango cha biashara kati ya China na Afrika kimekuwa kikiweka rekodi mpya ya juu, huku China ikidumisha nafasi yake ya kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 16 mfululizo.
Takwimu hizo za forodha zinaonesha kuwa mwaka 2024, kiwango cha biashara kati ya China na Afrika kilizidi Yuan trilioni 2 kwa mara ya kwanza (dola za Marekani takriban bilioni 291.94), kikifikia Yuan trilioni 2.1.
Aidha, takwimu hizo zinaonesha kuwa, katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, biashara ya China ya kuagiza na kuuza bidhaa kwa Afrika ilifikia Yuan bilioni 963.21, ongezeko la asilimia 12.4 kuliko kipindi kama hicho mwaka uliopita, na rekodi mpya ya juu katika historia kwa kipindi hicho.
Miongoni mwa hiyo, biashara ya China kuuza bidhaa kwa nchi za Afrika ilifikia Yuan bilioni 599.57, ongezeko la asilimia 20.2 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, huku ile ya kuagiza bidhaa kutoka nchi za Afrika ikifikia Yuan bilioni 363.64, ongezeko la asilimia 1.6, takwimu hizo zinaonesha.
Mamlaka hiyo ya Forodha imeeleza kuwa, tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2000, uhusiano kati ya pande hizo mbili umepiga hatua kubwa, na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara umeendelea kupanuka hadi kwenye ngazi ya juu zaidi na kujumuisha sekta nyingi zaidi.
Aidha, kielelezo cha Biashara kati ya China na Afrika kinachokusanywa na Forodha ya China kimepanda kwa kasi kutoka thamani ya msingi ya pointi 100 mwaka 2000 hadi kuvuka pointi 1000 mwaka 2023, na kufikia pointi 1056.53 mwaka 2024.
Mamlaka hiyo ya forodha imeeleza kuwa, kupanda huko kwa takwimu ni kiashiria cha wazi cha maendeleo ya kasi ya biashara yenye kustawi kati ya China na Afrika.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma