CEO wa Boeing asema angependa kuunga mkono uchunguzi kuhusu ajali ya ndege ya Boeing 787 nchini India

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2025

Waokoaji wakiwa wamebeba mwili wa wahanga kwenye eneo la ajali ya ndege ya Shirika Ndege la India mjini Ahmedabad, Jimbo la Gujarat, India, Juni 12, 2025. (Str/Xinhua)

Waokoaji wakiwa wamebeba mwili wa wahanga kwenye eneo la ajali ya ndege ya Shirika Ndege la India mjini Ahmedabad, Jimbo la Gujarat, India, Juni 12, 2025. (Str/Xinhua)

SAN FRANCISCO - Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Boeing Kelly Ortberg Amesema timu ya Boeing ingependa kuunga mkono uchunguzi unaoongozwa na Ofisi ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege ya India kuhusu ajali ya ndege ya Boeing 787, inayoendeshwa na Shirika la Ndege la India iliyokuwa ikisafiri kwenda London ikiwa na watu 242, wakiwemo marubani wawili na wafanyakazi 10, ambayo imetokea muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege katika Jimbo la Gujarat magharibi mwa India jana Alhamisi.

"Nimezungumza na Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la India N. Chandrasekaran ili kutoa uungaji mkono wetu kamili, na timu ya Boeing iko tayari kuunga mkono uchunguzi unaoongozwa na Idara ya Uchunguzi wa Ajali za Ndege ya India," Ortberg amesema katika taarifa baada ya ajali hiyo ya ndege ya Shirika la Ndege la India safari No. 171.

Kwa mujibu wa shirika hilo la ndege la India, ndege hiyo iliondoka Ahmedabad majira ya saa 7:38 Mchana kwa saa za India (0738 GMT).

Hii ni ajali ya kwanza kwa Boeing 787 Dreamliner, Mtandao wa Usalama wa Anga umeeleza.

Boeing imesema mapema Alhamisi katika taarifa nyingine kwamba kampuni hiyo inawasiliana na Shirika la Ndege la India kuhusu ajali hiyo ya ndege nchini India.

"Tunaendelea kuwasiliana na Shirika la Ndege la India kuhusu Ndege ya Safari No. 171 na tutawatoa msaada. Tuko pamoja na abiria, wafanyakazi, watu wa huduma ya kwanza na wote walioathirika," imesema kampuni hiyo katika taarifa hiyo.

"Rambirambi zetu za dhati zinaenda kwa wapendwa wa abiria na wafanyakazi waliokuwa ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la India Safari No. 171, vilevile kila mmoja aliyeathiriwa mjini Ahmedabad," Ortberg amebainisha.

Ortberg ameeleza kuwa, Boeing itatoa maelezo kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la India Safari No.171 kwa Ofisi ya Upelelezi wa Ajali za Ndege ya India (AAIB), kwa kuzingatia itifaki ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) inayojulikana kama Annex 13.

Watu wakitazama vifusi vya ndege ya Shirika la Ndege la India iliyoanguka katika eneo la Ahmedabad la Jimbo la Gujarat la India, Juni 12, 2025. (UNI/kupitia Xinhua)

Watu wakitazama vifusi vya ndege ya Shirika la Ndege la India iliyoanguka katika eneo la Ahmedabad la Jimbo la Gujarat la India, Juni 12, 2025. (UNI/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha