Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaonya hatari ya kutokea kwa baa la njaa nchini Sudan Kusini

(CRI Online) Juni 13, 2025

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) na Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF) yameonya Alhamisi kwenye ripoti ya pamoja kuwa baa la njaa linaweza kutokea katika kaunti mbili za Nasir na Ulang katika jimbo la Upper Nile, nchini Sudan Kusini ambazo zimeathiriwa vibaya na mapigano yanayoendelea na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu milioni 7.7 nchini humo, sawa na asilimia 57 ya jumla ya watu wake wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula kati ya mwezi Aprili hadi Julai.

Waziri wa usalama wa chakula na kilimo wa Sudan Kusini Bw. Hussein Abdelbagi Akol ametoa wito wa uratibu wa pande nyingi husika ili kukabiliana na njaa inayokumba watu hao walioathiriwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha