

Lugha Nyingine
Shughuli kubwa zaidi kati ya pande mbili za Mlango Bahari wa Taiwan kuhusu mawasiliano ya watu zafanyika
Wang Huning, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, akihutubia kwenye Baraza la 17 la Pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan mjini Xiamen, Mkoani Fujian, kusini mashariki mwa China, Juni 15, 2025. (Xinhua/Yao Daiwe)
XIAMEN - Mkutano mkuu wa Baraza la 17 la Pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan umefanyika jana Jumapili mjini Xiamen, Mkoani Fujian, China, ukianzisha shughuli mbalimbali ndani ya mfumokazi wake, ambapo chini ya kaulimbiu ya "kupanua mawasiliano ya watu na kuzidisha maendeleo jumuishi," Baraza hilo litafanya shughuli 56 za mawasiliano kuhusu ngazi ya umma, vijana, utamaduni na uchumi, likivutia watu zaidi ya 7000 kutoka sekta mbalimbali za Taiwan.
Wang Huning, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, alihudhuria mkutano huo, na kusisitiza umuhimu wa kulinda amani kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan na kushirikiana kuhimiza muungano wa taifa.
Wang amesema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 80 tangu ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupinga Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, vilevile kurejeshwa kwa Taiwan - hii ni kumbukumbu ya pamoja ya kitaifa kwa watu wa pande zote mbili za Mlango wa Bahari, akisisitiza kwamba matunda ya ushindi huo lazima yahifadhiwe.
“Pande zote mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan ni za China moja”, amesema, akisisitiza umuhimu wa kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na Maafikiano ya mwaka 1992.
Ametoa wito wa kupinga kithabiti shughuli za nguvu ya mafarakano ya kutaka “Taiwan ijitenge” na uingiliaji kutoka nje ili kulinda amani na utulivu wa Mlango wa Bahari kwa pamoja.
Wang amesisitiza kwamba China Bara siku zote itatoa uungaji mkono wa dhati kwa watu wa Taiwan na inafanya juhudi katika kuzidisha maendeleo jumuishi ya pande zote mbili za Mlango-Bahari ili kuwapa watu wa Taiwan hisia kubwa zaidi ya manufaa, furaha na kuwa sehemu yake.
Kabla ya mkutano huo, Wang alikutana na wageni kutoka Taiwan ambao wanahudhuria baraza hilo.
Ma Ying-jeou, mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Kuomintang cha China, pia alihudhuria mkutano huo na kusema kuwa maendeleo ya amani ya uhusiano kati ya Pande mbili za Mlango Bahari wa Taiwan ni matarajio ya pamoja ya watu wa pande zote mbili.
Ma ameelezea matumaini kwamba, juu ya msingi wa pamoja wa kisiasa wa kushikilia Maafikiano ya mwaka 1992 na kupinga "Taiwan ijitenge," mawasiliano na ushirikiano kati ya Pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan vitaimarishwa.
Wang Huning, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, akikutana Ma Ying-jeou na wageni wengine kutoka Taiwan kabla ya kufunguliwa kwa Baraza la 17 la Pande mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan mjini Xiamen, Mkoani Fujian, kusini mashariki mwa China, Juni 15, 2025. (Xinhua/Yao Daiwe)
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma