

Lugha Nyingine
Jeshi la Israel latangaza duru mpya ya mashambulizi ya anga katika vituo vya makombora vya Iran
Moshi ukifuka kwenda angani kufuatia mlipuko uliotokea Tehran, mji mkuu wa Iran, Juni 15, 2025. (Xinhua/Shadati)
JERUSALEM - Jeshi la anga la Israel limeanzisha duru mpya ya mashambulizi ya anga nchini Iran jana Jumapili usiku, yakilenga vituo vya makombora ya kurushwa kutoka chini kwenda kutua chini magharibi mwa nchi hiyo, Jeshi la Israel limetangaza katika taarifa na kusema kuwa mashambulizi hayo yamelenga kuharibu "malengo kadhaa” ya makombora.
Israel ilifanya mashambulizi makubwa zaidi ya anga dhidi ya Iran siku ya Ijumaa, ikipiga vituo vya nyuklia mjini Tehran na maeneo mengine kote nchini humo.
Shambulizi hilo limeua makumi ya wanasayansi, maafisa waandamizi wa usalama, na raia nchini Iran, na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi ya makombora na droni ambayo yameua watu takriban 14 nchini Israeli.
Jana Jumapili, Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alisema mashambulizi hayo ya anga yataendelea na yatalenga si tu vituo vinavyohusiana na nyuklia bali pia vituo vya makombora, maeneo ya kuzalisha silaha, mifumo ya ulinzi wa anga, na "maeneo lengwa ya serikali mjini Tehran."
Katika taarifa mpya kwa umma, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel "imedhamiria kutimiza lengo lake la kuondoa vitishio viwili" kutoka Iran.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma