

Lugha Nyingine
Jeshi la Sudan lazuia shambulizi la vikosi vya RSF dhidi ya El Fasher
Jeshi la Sudan (SAF) limesema kwamba wamezima shambulizi la wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) dhidi ya El Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, huku serikali ya mtaa ikiripoti kwamba watu watano wameuawa katika shambulizi la RSF dhidi ya makazi ya wakimbizi.
Divisheni ya sita ya askari wa ardhini ya SAF imetoa taarifa ikisema kuwa vikosi vya SAF vimeangamiza sehemu kubwa ya kikosi kilichofanya shambulizi, na kutoa pigo kubwa kwao ikiwa ni pamoja na kuteketeza magari ya kivita, na kusababisha makumi ya vifo na wengine wengi kujeruhiwa.
Wakati huo huo, Gavana wa Jimbo la Darfur Kaskazini Al-Hafiz Bakhit ametangaza kwamba wanamgambo wa RSF wameshambulia kwa mizinga makazi ya wakimbizi katika Wizara ya Kilimo na Rasilimali za Wanyama, na kusababisha vifo vya watu watano na wengine 30 kujeruhiwa.
RSF haijatoa tamko lolote kuhusu matukio ya El Fasher.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma