

Lugha Nyingine
Misri yaahirisha uzinduzi wa Jumba kubwa la Makumbusho la Misri kutokana na mivutano kati ya Israel na Iran
Picha hii iliyopigwa Juni 14, 2025 ikionyesha mwonekano wa Jumba kubwa la Makumbusho ya Misri katika eneo la karibu na Mapiramidi ya Giza mjini Giza, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
CAIRO - Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly alitangaza juzi Jumamosi kuwa Misri imeahirisha ufunguzi wa Jumba kubwa la Makumbusho la Misri (GEM) uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu kutokana na kuongezeka kwa makabiliano ya kijeshi kati ya Israel na Iran.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akizuru jimbo la kaskazini la Beheira, Madbouly amesema hali ilivyo sasa ya kikanda si mwafaka kuandaa tukio kubwa la kimataifa na kwamba ufunguzi wa jumba hilo la makumbusho, uliokuwa umepangwa awali kufanyika Julai 3, sasa utaahirishwa hadi robo ya nne ya mwaka huu.
"Mvutano wa kikanda unaweza kuendelea kwa wiki kadhaa....Tumegundua kuwa hatua inayopaswa kuchukuliwa ni kuahirisha tukio hili kubwa, ili liweze kuwa na msukumo mwafaka duniani na kufanyika katika mazingira yanayofaa" amesema, akiongeza kuwa tarehe mpya ya ufunguzi itatangazwa kufuatana na hali ya kikanda ya siku za baadaye.
Madbouly pia ametoa tahadhari kali kuhusu athari pana za mgogoro huo kati ya Israel na Iran, akisema hatari inayoongezeka ya makabiliano makubwa zaidi katika eneo zima la Mashariki ya Kati.
Likiwa linapatikana karibu na mapiramidi mashuhuri ya Giza na likienea kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba takriban 500,000, jumba hilo linadaiwa kuwa jumba kubwa zaidi la makumbusho ya kiakiolojia duniani linalojikita kwenye ustaarabu mmoja. Litakuwa na mabaki ya kale takriban 57,000, kwa mujibu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Misri.
Picha hii iliyopigwa Juni 14, 2025 ikionyesha mwonekano wa Jumba kubwa la Makumbusho la Misri katika eneo la karibu na Mapiramidi ya Giza mjini Giza, Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma