Maonyesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yafungwa na makubliano mengi kutiwa saini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2025

Muonyeshaji bidhaa (kulia) akipeana mkono na mtembeleaji kwenye Maonyesho ya nne ya   Uchumi na Biashara   ya China na Afrika kwenye Kituo cha Mikutano na Maonyesho ya Kimataifa cha Changsha  katika Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua/Chen Sihan)

Muonyeshaji bidhaa (kulia) akipeana mkono na mtembeleaji kwenye Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika kwenye Kituo cha Mikutano na Maonyesho ya Kimataifa cha Changsha katika Mkoa wa Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua/Chen Sihan)

CHANGSHA - Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yamefungwa jana Jumapili, huku makubaliano ya miradi jumla ya 176 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 11.39 yakitiwa saini wakati ambapo China na Afrika zikitafuta kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi, kamati ya maandalizi ya maonyesho hayo imetangaza jana Jumapili, ikisema kwamba takwimu hizo mbili ni ongezeko la asilimia 45.8 na asilimia 10.2 zaidi kuliko zile za maonyesho ya mwaka 2023.

Waandaaji wameeleza kuwa, hadi kufikia mchana wa jana Jumapili, watu zaidi ya 200,000 walikuwa wametembelea ukumbi mkuu wa maonyesho hayo mjini Changsha, mkoani Hunan katikati mwa China, idadi hiyo ya watembeleaji imeongezeka kwa mara dufu kuliko ile ya maonyesho yaliyopita.

Aidha, waandaaji wamesema kuwa, makubaliano yaliyosainiwa au yanayofikiwa kwa hatua ya mwanzo kwenye ukumbi mkuu yanakadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya yuan bilioni 2.5 (dola za Kimarekani karibu milioni 348).

Wameeleza kuwa, makubaliano yanayofikiwa kwa hatua ya mwanzo yenye thamani ya Yuan milioni 200 yametiwa saini kwenye maonyesho ya mashine nzito yaliyofanyika katika mji Xiangtan jirani wa Changsha.

Waandaaji wamesema kuwa, kwa mara ya kwanza, maonyesho hayo yalijumuisha maonyesho mahsusi kuhusu bidhaa maarufu za ushirikiano kati ya China na Afrika, bidhaa bora za Afrika, na viwanda vya mitindo vya China na Afrika.

“Kampuni takriban 2,100 zikiwemo 764 kutoka nchi 43 za Afrika zimeshiriki kwenye maonyesho hayo. Wanunuzi wa China na kimataifa walifikia 12,000 kwa idadi” waandaaji jana Jumapili walisema.

Habari zimesema kuwa, wakati wa maonyesho hayo ya siku nne, aina zaidi ya 200 za bidhaa za kilimo za Afrika ziliuzwa mtandaoni na katika supamaketi na kwamba nchi 14 za Afrika ziliandaa shughuli mahsusi za kutangaza uchumi na biashara.

Maonyesho hayo yameandaliwa kwa pamoja na serikali ya mkoa wa Hunan na Wizara ya Biashara ya China, yakivutia kampuni zaidi ya 4,700 za China na Afrika na washiriki 30,000 kushiriki kwenye maonyesho na mikutano.

China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 16 mfululizo hadi kufikia 2024, na ukuaji wa biashara ya pande mbili umeendelea kwa kasi mwaka 2025.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha