Teknolojia za nishati mpya za China zaunga mkono maendeleo ya kijani katika nchi za Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2025

CHANGSHA - Ushirikiano wa nishati ya kijani umejadiliwa sana katika maonesho ya 4 ya uchumi na biashara ya China na Afrika, yaliyofanyika mjini Chansha, mkoani Hunan katikati mwa China kuanzia Juni 12 hadi jana Jumapili Juni 15 ambapo kwenye maonyesho hayo, makubaliano mbalimbali ya ushirikiano katika mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua na magari yanayotumia umeme kati ya kampuni za China na Afrika yamesainiwa.

Kwenye ukumbi wa maonyesho ya nishati ya kijani wa maonyesho hayo, wawakilishi wa biashara walijadili uwezekano wa ushirikiano huku kukiwa na maonyesho ya mashine za kilimo, paneli za jua na magari maridadi yanayotumia umeme.

Picha hii iliyopigwa Juni 12, 2025 ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika mjini Changsha, Mkoani Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Chen Sihan)

Picha hii iliyopigwa Juni 12, 2025 ikionyesha hafla ya ufunguzi wa Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika mjini Changsha, Mkoani Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Chen Sihan)

Ufumbuzi wa Kuchaji wa EVS PLUS

Kwenye banda la maonyesho la Yadea ambayo ni kampuni ya vyombo vya usafiri vya magurudumu mawili vinavyotumia umeme, skuta zinazotumia umeme za rangi ya limau ya manjano na kijani kibichi zilivutia watu wengi. Vyombo hivi vyenye urefu wa mita 1.5 na uwezo wa kusafiri kilomita 130, vimetengenezwa kwa ajili ya hali ya barabara katika nchi za Afrika.

"Tunabadilisha miundo kuendana na mahitaji ya wenyeji, kama vile kuinua chassis kwa ajili ya matuta nchini Kenya ili kuhakikisha usalama na utulivu," amesema Zhang Yi, Mkurugenzi wa Uendeshaji Masoko wa Yadea Afrika Mashariki na Kusini.

China siku zote imetilia mkazo ushirikiano wa nishati na nchi za Afrika na kwa mujibu wa Mpango Kazi wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (2025-2027), China inahimiza uwekezaji katika miradi ya nishati mbadala barani Afrika.

Mtembeleaji maonyesho wa nchi za nje (kulia) akiwasiliana na muonyeshaji bidhaa kwenye Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Changsha mjini Changsha, Mkoani Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua/Chen Sihan)

Mtembeleaji maonyesho wa nchi za nje (kulia) akiwasiliana na muonyeshaji bidhaa kwenye Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonyesho cha Changsha mjini Changsha, Mkoani Hunan, katikati mwa China, Juni 13, 2025. (Xinhua/Chen Sihan)

Ushirikiano wa kivitendo wa nishati

Kwenye banda la Kampuni ya Teknolojia za Nishati Mpya ya Yingchen (YCSOLAR), kauli mbiu ya "Kutoa Ufumbuzi wa Mazingira yote ya Nishati ya Kijani" ilikuwa imebandikwa kwenye ubao wa nyuma.

Meneja wa Maendeleo ya Mradi wa Idara ya Biashara ya Ng'ambo ya kampuni hiyo Zhang Zixu alikuwa akitambulisha mfumo wa gridi ndogo wa PV-Uhifadhi Nishati-Diseli kwa wafanyabiashara wa Afrika.

Ukiwa umeundwa kushughulikia mapengo ya Afrika ya kufikia nishati katika maeneo ya mbali, mfumo huo unaunganisha vipengele vitatu vya msingi: safu za nishati ya jua kwa ajili ya uzalishaji umeme wakati wa mchana, mfumo wa betri ya kuhifadhi nishati kwa matumizi ya usiku, na mitambo ya dizeli kwa siku za mawingu na mvua.

Katika vitongoji vya mji wa Kano, Nigeria, ambapo umeme wa gridi kwa kila siku mara nyingi hupatikana kwa saa nne tu, mjasiriamali ameshirikiana na YCSOLAR kuwasha umeme kwenye kituo cha kusindika ufuta.

Ufungaji wa gridi ndogo sasa unawezesha ratiba ya kufanya kazi ya saa 22 kila siku, ikibadilisha kiwanda hicho kuwa nguvu mpya ya kutoa mchango kwa ajili ya uchumi wa wenyeji.

Mtembeleaji maonyesho akipiga picha za gari la usafi wa mazingira kutoka kampuni ya teknolojia ya mazingira ya China ya Infore Enviro kwenye Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika mjini Changsha, Mkoani Hunan, katikati mwa China, Juni 12, 2025. (Infore Enviro/kupitia Xinhua)

Mtembeleaji maonyesho akipiga picha za gari la usafi wa mazingira kutoka kampuni ya teknolojia ya mazingira ya China ya Infore Enviro kwenye Maonyesho ya nne ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika mjini Changsha, Mkoani Hunan, katikati mwa China, Juni 12, 2025. (Infore Enviro/kupitia Xinhua)

Kuchangia uzoefu wa usimamizi wa mazingira mjini

Katika mji mkuu wa Ghana, Accra, magari ya usafi wa mazingira kutoka kampuni ya teknolojia ya mazingira ya China ya Infore Enviro yanafanya kazi kimya kabla ya mapambazuko, kwa ufanisi yakisafirisha takataka kwa njia iliyopangwa mapema.

Zhang Hengsen, mkurugenzi wa mauzo wa Idara ya Biashara ya Ng'ambo ya Infore Enviro, anajivunia kwamba kampuni hiyo imetoa mchango katika kuboresha teknolojia ya usafi wa mazingira mijini na muundo wa uendeshaji.

Katika miongo miwili iliyopita, idadi ya magari ya Infore Enviro yanayofanya kazi nchini Ghana imeongezeka kutoka mia moja hadi karibu elfu, na kampuni imepata imani ya wenyeji kupitia kutegemewa, ufanisi wa hali ya juu wa usafiri na mifumo ya kisasa ya kusafisha.

"China inawezesha Afrika kubadilisha muundo wake wa uchumi wa kijani kwa kutoa bidhaa zenye bei nafuu, huku ushirikiano ukienea zaidi ya mauzo ya nje ya vifaa kujumuisha uhamishaji wa maarifa na mafunzo ya ustadi kwa wenyeji -- kwa lengo la kuwezesha bara la Afrika kujenga maendeleo endelevu ya kijani." Amesema Xu Xiangping, mkuu wa Baraza la Kuhimiza Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha