

Lugha Nyingine
China, Kazakhstan kuimarisha uhusiano na kuhimiza maendeleo na amani ya kikanda na kimataifa
Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakifanya mazungumzo katika ikulu ya rais mjini Astana, Kazakhstan, Juni 16, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
ASTANA - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu alipokutana na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev kabla ya mkutano wa pili wa kilele wa China na Asia ya Kati amesema kuwa China inapenda kushirikiana na Kazakhstan katika kuchangia zaidi amani na maendeleo ya kikanda na dunia kwa utulivu na nguvu chanya ya uhusiano wa pande hizo mbili.
Rais Xi ameeleza kuwa uhusiano kati ya China na Kazakhstan umestahimili majaribu ya mabadiliko ya kimataifa na umekuwa ukidumisha siku zote maendeleo ya kiwango cha juu kutokana na ukaribu wa kijiografia na urafiki wa muda mrefu kati ya watu wao, na pia ni chaguo la lazima la nchi hizo mbili kwa kutafuta maendeleo kwa pamoja.
Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni chini ya upangaji wa pamoja wa viongozi hao wawili, jumuiya ya China na Kazakhstan yenye mustakabali wa pamoja imehusisha mambo mengi mbalimbali, na matokeo halisi na yanayoweka kipaumbele kwa watu yanapatikana siku hadi siku yakiongeza hisia za kujivunia za watu wa pande hizo mbili.
"China daima imekuwa ikiutendea na kuendeleza uhusiano wake na Kazakhstan kutoka kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na inapenda kufanya juhudi za pamoja na Kazakhstan ili kuimarisha kithabiti urafiki kati ya nchi hizo mbili" amesema.
Rais Xi amesisitiza kuwa, China na Kazakhstan kila moja iko katika kipindi chake muhimu cha maendeleo na ustawishaji, na nchi hizo mbili zinapaswa kufanya juhudi kwa pamoja ili kusukuma mbele ushirikiano wa pande zote.
Kwanza, Rais Xi amependekeza kuwa, kuaminiana kimkakati kwenye ngazi ya juu kunapaswa kuongoza maendeleo ya uhusiano wa pande mbili, pili, kufanya pamoja ujenzi wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kuinua kiwango cha ushirikiano wa pande mbili, tatu, kuanzisha ushirikiano wa usalama katika mambo yote ili kulinda amani na utulivu wa nchi hizo mbili, na nne, kufanya mawasiliano ya aina mbalimbali kati ya watu na watu ili kuimarisha zaidi msingi wa urafiki kati ya China na Kazakhstan.
Kwa upande wake, Rais Tokayev amesema kuwa China ni jirani mwema , rafiki wa karibu na mshirika wa uhakika wa Kazakhstan.
Amesema uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati ulio wa kudumu na wa pande zote kati ya Kazakhstan na China unaingia katika zama mpya za dhahabu, ukisukuma mbele maendeleo endelevu ya uchumi na jamii ya nchi hizo mbili, ukinufaisha watu wa pande hizo mbili, na kuwa mfano wa kuigwa wa uhusiano kati ya nchi na nchi.
Kufuatia mazungumzo hayo, wakuu hao wa nchi walishuhudia mabadilishano ya nyaraka zaidi ya 10 za ushirikiano wa pande mbili katika sekta za biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, forodha, utalii na vyombo vya habari.
Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakitembea kuelekea ikulu ya rais mjini Astana, Kazakhstan, Juni 16, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev wakifanya mazungumzo katika ikulu ya rais mjini Astana, Kazakhstan, Juni 16, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev katika ikulu ya rais mjini Astana, Kazakhstan, Juni 16, 2025. (Xinhua/Li Tao)
Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev katika ikulu ya rais mjini Astana, Kazakhstan, Juni 16, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma