Iran yapiga makombora mapya kadhaa dhidi ya Kaskazini mwa Israel

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2025

Picha iliyopigwa Juni 16, 2025 ikionyesha mabaki ya kombora mjini Safed, kaskazini mwa Israel. (David Cohen/JINI kupitia Xinhua)

Picha iliyopigwa Juni 16, 2025 ikionyesha mabaki ya kombora mjini Safed, kaskazini mwa Israel. (David Cohen/JINI kupitia Xinhua)

JERUSALEM - Makombora kadhaa kutoka Iran yamerushwa dhidi ya Israel jana Jumatatu jioni, yakisababisha milio ya ving'ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga mjini Haifa na katika miji mingi na maeneo ya makazi kaskazini mwa Israel na Uwanda wa juu wa Golan inayokaliwa na Israel, Jeshi la Israel limesema.

Shirika la Magen David Adom la Israel limesema hakuna ripoti za mara moja za majeruhi.

Kituo cha habari cha televisheni cha Kan cha serikali ya nchi hiyo kimeripoti kuwa makombora matatu yalirushwa kutoka Iran, moja kati yao limezuiliwa na jeshi na mengine mawili yameangukia kwenye viwanja vya wazi.

Kituo hicho kimeeleza kuwa vipande vya kombora vilianguka katika eneo la Safed, vikizua moto.

Shambulizi hilo la makombora lililofanywa na Iran dhidi ya Israel baada ya Israel iliyokuwa imefanya mashambulizi ya anga ya kushtukiza na ya kuua siku ya Ijumaa dhidi ya Iran.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha