

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa Israel asema Israel imedhibiti anga ya Tehran
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa taarifa jana Jumatatu akisema kuwa jeshi la anga la Israel linadhibiti anga ya Tehran, mji mkuu wa Iran, hali ambayo “inabadilisha vita hivyo”.
Wakati huohuo Mshauri Mwandamizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi amesema jeshi lake liko tayari kwa vita kamili na ya muda mrefu na Israel.
Katika taarifa yake hiyo, Netanyahu amesema jeshi la Israel liko kwenye mchakato wa kutimiza lengo la kukomesha matishio ya silaha za nyuklia na makombora ya Iran, ambapo Israel imetoa tahadhari kwa wakazi wa Tehran kuondoka.
Vyombo vya habari vya Iran vimemnukuu Vahidi akisema kuwa IRGC imefikiria uwezekano wa aina zote, na iko tayari kukabiliana na hali yoyote kwenye vita.
Ameongeza kuwa IRGC bado haijatumia vya kutosha uwezo wake wa makombora, na kwamba itatumia silaha za kisasa kwenye vita hivyo katika wakati mwafaka, yakiwemo makombora ya kizazi kipya.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma