Baraza Kuu la UM laitangaza Desemba 4 kuwa siku ya kimataifa dhidi ya hatua za kulazimisha zinazotolewa na upande mmoja

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2025

Sophia Yohannes, Balozi wa Eritrea katika Umoja wa Mataifa, akiwasilisha mswada wa azimio kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 16, 2025. (Manuel Elias/Picha ya Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

Sophia Yohannes, Balozi wa Eritrea katika Umoja wa Mataifa, akiwasilisha mswada wa azimio kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 16, 2025. (Manuel Elias/Picha ya Umoja wa Mataifa/kupitia Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Jumatatu limepitisha azimio la kuitangaza Desemba 4 kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa Dhidi ya Hatua za Kulazimisha za Upande Mmoja.

Azimio hilo linahimiza nchi mbalimbali kujiepusha, kupitisha, kutangaza na kutumia hatua zozote za upande mmoja za kiuchumi, kifedha au kibiashara ambazo si kwa mujibu wa sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa ambazo zinazuia au kuharibu mafanikio kamili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hasa katika nchi zinazoendelea.

Linaelezea imani kwamba kuanzishwa kwa Siku hiyo ya Kimataifa kutakamilisha juhudi zinazoendelea kwa kulenga kuongeza ufahamu wa kimataifa juu ya athari mbaya za hatua za kulazimisha za upande mmoja na kuhimiza ushirikiano na mshikamano mkubwa zaidi wa kimataifa kati ya nchi mbalimbali katika kushughulikia matokeo ya hatua hizo.

Azimio hilo limepitishwa kwa kura 116 za ndiyo, 51 za hapana na 6 hazikupiga. Nchi za Kaskazini, zikiwemo nchi za EU na Australia, Uingereza, Canada, Japan, Marekani, zimepiga kura ya hapana dhidi ya azimio hilo.

Azimio hilo linamuomba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua na mipango muhimu kwa Umoja wa Mataifa kuadhimisha na kutangaza Siku hiyo ya Kimataifa, ikiwemo kama sehemu ya jitihada za kimataifa za kuongeza ufahamu kuhusu athari mbaya za hatua za kulazimishwa za upande mmoja zisizozingatia sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo linaalika nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa na waangalizi, mashirika ya mfumo wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa na ya kikanda, vilevile mashirika ya kiraia, watu binafsi na wadau wengine husika kuadhimisha Siku hiyo ya Kimataifa na kuongeza ufahamu wa athari mbaya za hatua za kulazimishwa za upande mmoja zisizozingatia sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa, hasa kwa nchi zinazoendelea.

Linamwomba Rais wa Baraza Kuu kuandaa mkutano usio rasmi wa wajumbe wote kuadhimisha na kutangaza Siku hiyo ya Kimataifa kila mwaka kuanzia mwaka 2025.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha