Rais wa Guinea-Bissau azindua barabara kuu iliyojengwa kwa ufadhili wa China

(CRI Online) Juni 17, 2025

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo jana Jumatatu aliongoza hafla ya uzinduzi wa barabara kuu inayounganisha mji mkuu wa nchi hiyo, Bissau na kitongoji chake cha Safim, ikiwa na umbali wa kilomita 8.2.

Barabara hiyo kuu imejengwa na kampuni ya barabara na madaraja ya Longjian ya China, na kufadhiliwa kikamilifu na serikali ya China kwa gharama ya dola za Kimarekani milioni 30.

Kwenye hafla hiyo ya uzinduzi, Rais Embalo amesema kuwa barabara hiyo ni alama ya urafiki mkubwa, mshikamano, na ushirikiano unaoendelea kati ya Guinea-Bissau na China.

Balozi wa China nchini Guinea-Bissau Yang Renhuo amesisitiza dhamira ya China ya kuendelea kuiunga mkono Guinea-Bissau katika miradi yake ya maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha