

Lugha Nyingine
Ufundi wa kijadi wa kutengeneza tofu wahimiza ukuaji wa viwanda vya Mji Huainan, China (5)
Katika maelfu ya miaka iliyopita, ufundi wa kijadi wa kutengeneza tofu umekuwa ukirithishwa kizazi hadi kizazi katika Tarafa ya Bagongshan ya Wilaya ya Shouxian ya Mji wa Huainan katika Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. Mwaka 2014 ufundi huo umewekwa kwenye kundi la nne la orodha wakilishi ya kitaifa ya mali ya urithi wa utamaduni usioshikika wa China.
Mchakato wa ajabu wa kutoka maharagwe ya soya hadi tofu unahusisha kazi zaidi ya kumi kama vile kuchagua soya, kuloweka, kusaga, kuchemsha maziwa ya soya na kutengeneza mabonge.
Katika mji huo wa Huainan, tofu inaweza kutengenezwa kuwa mamia ya vitoweo vikiwemo jiaozi (dumplings) za tofu, mshikaki wa tofu ya kukaangwa ya Huainan na "tofu yenye umbo la maua ya Chrysanthemum", ambayo inahitaji mpishi kufanya kazi ya kukata kipande cha tofu kwa zaidi ya mara 160.
Mwaka 2024, thamani ya uzalishaji wa mnyororo mzima wa shughuli za kutengeneza vyakula vya soya katika mji huo ilifikia yuan bilioni 4.52 (dola za kimarekani kama bilioni 0.63), na kupata ongezeko la asilimia 10.4 kuliko mwaka 2023.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma