Shughuli ya “Matunda ya ASEAN kukusanyika Guangxi” yafanyika mjini Nanning, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2025

Picha ikionesha eneo la shughuli. (Picha kwa hisani ya waandaaji)

Picha ikionesha eneo la shughuli. (Picha kwa hisani ya waandaaji)

Shughuli ya “Matunda ya ASEAN Kukusanyika Guangxi, Kufanya Ununuzi Kupitia RCEP Kuwa Rahisi na Bora— Fanya Manunuzi katika Kituo cha Guangxi China” imezinduliwa jana Jumatano, tarehe 18 Juni katika Kituo cha Kukusanyika Bidhaa Maalum za China—ASEAN kilichopo mjini Nanning, Guangxi, China.

Guangxi ni dirisha la China la kufungua mlango na ushirikiano na nchi za ASEAN, vilevile mkoa wenye uzalishaji mkubwa zaidi wa matunda nchini humu, na “lango kuu” kwa matunda ya ASEAN kuingia China, ikijulikana kama "kikapu cha matunda" cha nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaji, lengo la kufanyika shughuli hiyo ni kuwezesha kutumia kikamilifu nafasi ya Guangxi kama kituo cha kwanza na lango muhimu kwa matunda ya ASEAN na bidhaa bora za RCEP kuingia kwenye soko la China, na kusukuma mbele kutimizwa kwa dira ya “kuzalishwa ASEAN, kusambazwa Guangxi, na kuuzwa vizuri China.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, katika shughuli hiyo, mabalozi kutoka nchi 8 zikiwemo Vietnam, Brunei, Cambodia, na Indonesia walinadi matunda ya nchi zao na bidhaa bora za RCEP kupitia ana kwa ana, au kwa njia ya video.

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa, mfumo mkubwa wa AI wa Matunda ya ASEAN-China (Guangxi) ulizinduliwa rasmi kwenye eneo la shughuli hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa, Guangxi itaendeleza kwa kina ushirikiano wa uchumi na biashara ya matunda na nchi za ASEAN, kuhimiza uunganishaji wa miundombinu, kujenga mfumo bora na wenye ufanisi wa wa forodha wa kuidhinisha bidhaa zinazoagizwa na kuuzwa nje, na kwa pamoja kufungua nafasi ya soko la biashara ya matunda kati ya China na ASEAN.

Matunda kutoka nchi za ASEAN yakiuzwa kwenye shughuli. (Picha kwa hisani ya waandaaji)

Matunda kutoka nchi za ASEAN yakiuzwa kwenye shughuli. (Picha kwa hisani ya waandaaji)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha