

Lugha Nyingine
Maonyesho ya picha yafanyika Russia kuadhimisha ushindi wa Vita vya Dunia dhidi ya Ufashisti
Fu Hua, Mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua, na Andrey Kondrashov, mkurugenzi mkuu wa shirika la habari la Russia, TASS, kwa pamoja wakizindua maonyesho ya picha ya kumbukumbu ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti mjini St. Petersburg, Russia, Juni 19, 2025. (Xinhua/Cao Yang)
ST. PETERSBURG, - Maonyesho ya picha yenye kaulimbiu ya "Sifa za Kudumu, Kumbukumbu ya Milele" kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti yameanza mjini St. Petersburg, Russia jana Alhamisi ambapo maonyesho hayo yameandaliwa kwa pamoja na Shirika la Habari la China, Xinhua na shirika la habari la la Russia, TASS.
Fu Hua, Mkuu wa Shirika la Habari la China Xinhua, na Andrey Kondrashov, mkurugenzi mkuu wa shirika la habari la Russia TASS, kwa pamoja wamezindua maonyesho hayo.
Fu amesema kuwa maonyesho hayo yanalenga kurejelea historia, kupata mafunzo kutoka siku za nyuma, kukumbuka mashujaa walioaga dunia, na kuenzi urafiki wa pande mbili.
“Xinhua inafanya juhudi kuzidisha zaidi mawasiliano na maingiliano na TASS, kutafuta fursa za shughuli nyingi zaidi za mawasiliano ya kitamaduni, na kutoa sauti za pamoja kwenye jukwaa la kimataifa,” Fu ameongeza.
Kwa upande wake Kondrashov amezungumzia ushirikiano wa muda mrefu na wenye matunda kati ya TASS na Xinhua, akisema kuwa maonyesho hayo si tu yanaonesha ushirikiano wa ngazi ya juu wa mashirika hayo mawili, bali pia yanasisitiza ukumbusho wa historia ya pamoja.
“Picha zinazoonyeshwa zinarekodi baadhi ya watu na matukio muhimu, ikitukumbusha kwamba ni lazima tukumbuke historia. Russia itasimama kidete na China ili kukumbuka historia kwa pamoja,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova, amesema kwenye hafla ya ufunguzi.
Maonyesho hayo yanaonyesha matukio ya watu wa China na Russia wakipigana bega kwa bega na kuungana mkono katika Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, yakiangazia mchango wa kihistoria wa nchi hizo mbili katika kulinda amani ya dunia na harakati ya maendeleo ya binadamu.
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma