Jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini lafanya Siku ya Maombolezo huku idadi ya waliofariki kwa mafuriko ikifikia 92

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2025

Watu wakiwa wamekusanyika kuomboleza watu waliofariki kwenye mafuriko mjini Mthatha, Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini, Juni 19, 2025. (Serikali ya Jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini/kupitia Xinhua)

Cape Town - Jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini limefanya Siku ya Maombolezo ya kijimbo jana Alhamisi ili kutoa heshima kwa watu waliofariki katika mafuriko makubwa yaliyotokea wiki iliyopita, huku idadi ya waliofariki ikiongezeka hadi kufikia 92.

Ibada hiyo ya kumbukumbu iliyofanyika katika Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Kazi cha King Sabatha Dalindyebo mjini Mthatha, ambapo viongozi wa serikali na wanajamii wanakusanyika pamoja kutoa heshima kwa watu waliopoteza maisha na kutoa rambirambi na pole kwa familia zilizofiwa.

"Kwa sasa, idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na hali mbaya ya hewa imefikia 92 katika sehemu mbalimbali za Eastern Cape na hii ikiwemo pamoja na mwili wa msichana mdogo uliopatikana kando ya Mto Mthatha mapema jioni hii (juzi Jumatano jioni)," taarifa iliyotolewa juzi Jumatano usiku na Serikali ya Jimbo la Eastern Cape imeeleza

Mthatha, iliyoko katika Manispaa ya Wilaya ya OR Tambo bado ni eneo lililoathirika zaidi katika jimbo lote, na mamlaka zimeonya kuwa huenda idadi ya vifo itaendelea kuongezeka, taarifa hiyo imesema.

"Jukumu letu la pamoja la haraka ni kushirikiana na familia zilizofiwa ili kuhakikisha watu 92 waliopoteza maisha katika balaa wanazikwa kwa heshima," Waziri Mkuu wa Jimbo la Easten Cape Lubabalo Oscar Mabuyane amesema kwenye ibada hiyo ya kumbukumbu. "Baada ya hapo, tunafanya juhudi pamoja kuanza mchakato wa kujenga upya maeneo ya makazi yaliyoathirika."ameeleza.

Waziri Mkuu huyo amesema kuwa, watu zaidi ya 4,300 wameathiriwa katika mafuriko, nyumba 4,229 zilibomolewa na nyingine 1,963 kupata uharibifu wa sehemu ya paa.

“Wakati huo huo, jumla ya shule 413 zimepata uharibifu, ikiathiri vyumba vya madarasa 1,471 na kuvuruga elimu kwa wanafunzi takriban 48,341, amesema,” na bado "hatujaorodhesha uharibifu wa barabara, madaraja, hospitali na miundombinu ya maji lakini kwa sasa tunakadiria uharibifu huo kuwa wenye thamani ya randi bilioni 4 za Afrika Kusini (Dola za Kimarekani takriban milioni 220).

Mabuyane pia ameonya kwamba maafa hayo ya hivi karibuni lazima yawe tahadhari ya kuamsha. "Kuna masomo mengi ambayo sote tunapaswa kujifunza kutokana na janga la aina hii. Hata hivyo, leo nataka kusisitiza hali halisi ya mabadiliko ya tabianchi," amesema. "Haitoshi tena kuchukua hutua kwa majanga. Ni lazima tujiandae kuyakabili na kuyazuia kwa kadiri inavyowezekana."

Watu wakiwa wamekusanyika kuomboleza watu waliofariki kwenye mafuriko mjini Mthatha, Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini, Juni 19, 2025. (Serikali ya Jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini/kupitia Xinhua)

Watu wakiwa wamekusanyika kuomboleza watu waliofariki kwenye mafuriko mjini Mthatha, Jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini, Juni 19, 2025. (Serikali ya Jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha