UN yahimiza uungaji mkono zaidi kwa manusura na waathirika wa ukatili wa kingono nchini Somalia

(CRI Online) Juni 20, 2025

Umoja wa Mataifa umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Ukatili wa Kingono katika Vita nchini Somalia jana Alhamis kwa kutoa wito wa uungaji mkono zaidi kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kingono.

"Kwa Somalia kujenga jamii isiyo na unyanyapaa na mifadhaiko ya ukatili wa kingono, sote lazima kufanya kazi pamoja kuzuia na kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kingono” Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia James Swan amesema katika taarifa iliyotolewa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Siku ya Kimataifa ya Kuondoa Ukatili wa Kingono katika Vita huadhimishwa Juni 19 kila mwaka. Inatumika kama kikumbusho cha wajibu wa pamoja wa jumuiya ya kimataifa katika kuzuia na kumaliza ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro, na kudumisha hadhi na haki za binadamu kwa wote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha