

Lugha Nyingine
Rais wa Uganda ahimiza raia kukataa rushwa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2026
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa wito kwa raia kukataa rushwa ya wapiga kura kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa nchi hiyo mwaka 2026.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano jioni na Ikulu ya Uganda, Rais Museveni amewahimiza Waganda kusimama dhidi ya rushwa na kufanya maamuzi ya kiuchaguzi kwa msingi wa kanuni na maslahi ya taifa, badala ya motisha za kifedha za muda mfupi ambazo zinaweza kudhoofisha matokeo ya kidemokrasia.
Rais huyo ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kuhitimisha Ziara ya Kikanda ya Muundo wa Maendeleo ya Parishi (PDM) katika Kaunti ndogo ya Kituntu, iliyoko wilaya ya kati ya Mpigi, akisisitiza kuwa serikali imetekeleza hatua za kuzuia wizi wa kura.
Amebainisha kuwa katika uchaguzi wa 2021, upinzani uliiba kura milioni 2.7 kutokana na uzembe wa baadhi ya wanachama wa chama tawala, akibainisha kuwa sasa wameanzisha mashine za kibayometriki ili kuhakikisha kila mtu anapiga kura mara moja.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Uganda, uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais na ubunge utafanyika kati ya Septemba 17 na Oktoba 3. Kampeni zimepangwa kuanza wiki ya pili ya Oktoba, huku upigaji kura wa kumchagua rais na wabunge ukiwa umepangwa Januari 12, 2026.
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma