Wataalam wasema ushirikiano na China umeendeleza amani na utulivu katika Pembe ya Afrika

(CRI Online) Juni 20, 2025

Uwekezaji wa China katika miradi ya kiuchumi na kijamii umechochea juhudi za kuelekea maendeleo ya mambo ya kisasa katika Pembe ya Afrika, ambayo migogoro na athari za tabianchi zimekuwa zikizuia juhudi za maendeleo za nchi za kanda hiyo.

Hayo yamesemwa na wataalam waliokutana kwenye Semina ya tatu ya Mtazamo wa Amani na Maendeleo katika Pembe ya Afrika iliyofanyika Alhamisi mjini Nairobi, Kenya.

Ikiwa imefanyika chini ya kaulimbiu ya "Maendeleo ya Mambo ya Kisasa ya China na Afrika na Ukanda wa Kiuchumi wa SGR", semina hiyo imeandaliwa na Ubalozi wa China nchini Kenya na Taasisi ya Sera ya Afrika, na kuhudhuriwa na watunga sera waandamizi, wanadiplomasia, wasomi na watendaji wa sekta hiyo, huku ikisisitiza umuhimu wa miradi ya miundombinu inayofadhiliwa na China katika Pembe ya Afrika.

Akiongea kwenye semina hiyo, mjumbe maalum wa masuala ya Pembe ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Xue Bing, amesema Beijing imekuwa ikiunga mkono juhudi za pande nyingi za kufikia maendeleo ya muda mrefu, amani na utulivu katika kanda hiyo.

Naye mtendaji mkuu wa Taasisi ya Sera ya Afrika, Peter Kagwanja, amesema utatuzi wa migogoro lazima uwe kiini cha juhudi za kujenga upya uchumi katika eneo la Pembe ya Afrika ambalo limeharibiwa na migogoro na majanga ya asili ambayo yamekuwa yakindelea kwa miongo kadhaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha