Zambia yasitisha majaribio ya chanjo dhidi ya VVU baada ya Marekani kuondoa ufadhili

(CRI Online) Juni 20, 2025

Vyombo vya habari vya Zambia vimeripoti Alhamisi kuwa mamlaka ya afya ya Zambia imesitisha majaribio ya kimatibabu yaliyopangwa ya chanjo dhidi ya VVU baada ya Marekani kuondoa ufadhili.

Mwezi Januari, Mamlaka ya Taifa ya Usalama wa Kibiolojia ya Zambia iliidhinisha majaribio ya kimatibabu ya chanjo hiyo dhidi ya VVU kufanyika katika Kituo cha Utafiti wa Afya ya Familia cha Zambia (CFHRZ), chini ya ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

Hata hivyo, mkurugenzi wa mradi katika CFHRZ William Kilembe amethibitisha kuwa majaribio hayo yamesitishwa mwezi Februari kutokana na ukosefu wa fedha kutoka USAID.

Ameongeza kuwa shughuli zote zimesitishwa, zikiwemo za utafiti na mpango wa chanjo, na kazi nyingine husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha