

Lugha Nyingine
China yalaani vikali mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran
BEIJING - China inalaani vikali mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran na upigaji mabomu wake dhidi ya vituo vya nyuklia vilivyo chini ya uangalizi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China amesema jana Jumapili alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba Marekani imefanya mashambulizi dhidi ya vituo vitatu vya nyuklia nchini Iran.
Msemaji huyo amesema, "Hatua za Marekani zimekiuka vibaya nia na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, na kuifanya hali ya Mashariki ya Kati izidi kuwa mbaya," China inatoa wito kwa pande husika, hasa Israel, kusimamisha vita haraka iwezekanavyo, kuhakikisha usalama wa raia, na kuanza mazungumzo na majadiliano.
Msemaji huyo amesema China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kufanya juhudi pamoja na kulinda haki, na kufanya jitahidi zaidi kwa ajili ya kurejesha amani na utulivu katika Mashariki ya Kati.
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma