

Lugha Nyingine
Rais wa Iran aionya Marekani juu ya kulipiza kisasi baada ya mashambulizi kwenye maeneo ya nyuklia
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian akihudhuria mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, Septemba 16, 2024. (Xinhua/Shadati)
TEHRAN - Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema kwamba Marekani lazima "ipokee ulipizaji kisasi kwa uvamizi wake," kufuatia mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran ambapo katika kujibu wito wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wa kujizuia, Rais Pezeshkian amesema Marekani lazima ikabiliane na matokeo kwa mashambulizi yake hayo dhidi ya Iran.
Ameyaelezea mashambulizi hayo ya Marekani kuwa ni "ishara wazi ya kukosa kwake udhati na kutokuwa na msingi wa madai yake kuhusu kufanya mazungumzo na kutafuta amani."
Pamoja na hayo, Rais Pezeshkian amesisitiza kuwa Iran itaendelea kufanya ushirikiano wa kidiplomasia na Ulaya.
"Siku zote tumetangaza nia yetu ya kufanya mazungumzo na Ulaya na hatujawahi kuacha njia ya diplomasia, kwani tunashikilia kuwa hakuna anayeweza kupata madhara yoyote kutokana na mazungumzo." Rais Pezeshkian amesema kwenye mazungumzo ya simu na Rais Macron, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi yake.
Kwenye mazungumzo hayo, Rais Macron amesisitiza nia ya Ufaransa kufanya mazungumzo na Iran na kusema ufaransa itaendeleza juhudi za kusitisha mgogoro huo na kurejesha utulivu, kwa mujibu wa taarifa hiyo.
Rais Donald Trump wa Marekani juzi Jumamosi alitangaza kwenye Mtandao wa True Social kwamba majeshi ya Marekani yamekamilisha mashambulizi kwenye maeneo matatu ya nyuklia ya Iran, ambayo ni Fordow, Natanz, na Isfahan.
Mashambulizi hayo ya Marekani yamefuatia mashambulizi ya Israel yaliyoanzishwa tangu Juni 13 katika maeneo mbalimbali lengwa nchini Iran, yakiwemo maeneo ya nyuklia na kijeshi, yakiua makamanda kadhaa waandamizi, wanasayansi wa nyuklia na raia.
Iran imekuwa ikilipiza kisasi kwa mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya Israel. Hadi kufikia Jumamosi, watu zaidi ya 400 walikuwa wameshauawa na zaidi ya 3,500 kujeruhiwa nchini Iran, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Iran. Nchini Israeli, mamlaka zimeripoti vifo vya watu 24.
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma