Vikosi vya Somalia na AU vyachukua tena udhibiti wa maeneo ya kimkakati kutoka kundi la Al-Shabab

(CRI Online) Juni 23, 2025

Ujumbe wa Umoja wa Afrika wa Kuleta Uungaji Mkono na Utulivu nchini Somalia (AUSSOM) umesema, vikosi vyake kwa kushirikiana na jeshi la Somalia (SNAF) vimechukua tena udhibiti wa maeneo ya kimkakati ya Sabiid na Anole kutoka kundi la Al-Shabab.

AUSSOM imesema kwenye taarifa iliyotolewa jana Jumapili mjini Mogadishu kuwa, hatua hiyo inafuatia operesheni ya pamoja ya siku tatu iliyoitwa “Dhoruba ya Kimya” (Silent Storm), ambayo inalenga kukomboa maeneo yanayoshikiliwa na kundi la Al-Shabab katika Jimbo la Lower Shabelle nchini humo.

Kamanda wa sekta ya kwanza ya AUSSOM Bw. Joseph Ssemwanga amesema, operesheni hiyo itaendelea katika majimbo ya Middle Shabelle, hadi matishio ya kundi la Al-Shabab yatakapokuwa yameondolewa kikamilifu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha