Timu ya madaktari wa China yatoa huduma za afya bila malipo kwa watoto yatima zaidi ya 200 wa Zanzibar

(CRI Online) Juni 23, 2025

Kundi la 34 la Timu ya ya madaktari wa China waliopo Tanzania Zanzibar limetoa huduma ya afya bila malipo kwa watoto yatima zaidi ya 200 na wafanyakazi katika kituo cha watoto yatima cha visiwani humo.

Madaktari wa China kutoka idara mbalimbali, ikiwemo upasuaji, magonjwa ya wanawake na meno, wamefanya uchunguzi wa kina wa mwili kwa watoto na wafanyakazi katika kituo hicho, na kutoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kituo hicho kuhusu huduma za mwendelezo na utaratibu wa matibabu kwa wale waliokutwa na magonjwa.

Kiongozi wa timu hiyo Chen Wei amesema, kupitia shughuli hiyo, wanatarajia si tu kulinda afya ya watoto na wafanyakazi hao, bali pia kuwashawishi kukabiliana na maisha kwa ujasiri na kutimiza ndoto zao.

Naye ofisa ushirikiano wa sekta ya afya katika Wizara ya Afya Zanzibar, Mariam Khalfan amesema madaktari wa China wamerejesha matumaini kwa watoto yatima wa Zanzibar na kupanda mbegu ya urafiki ambayo inaendelea kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha