Rais wa Tanzania azindua daraja lililojengwa na China kwenye Ziwa Victoria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2025

Picha iliyopigwa Juni 19, 2025 ikionyesha Daraja Magufuli lililojengwa na Kampuni ya China mjini Mwanza, Tanzania. (Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China/kupitia Xinhua)

MWANZA, Tanzania - Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amezindua Daraja Magufuli lililojengwa na kampuni ya China, linalovuka Ziwa Viktoria na likisimama kama daraja refu zaidi linaloshikiliwa kwa kebo barani Afrika ambapo katika hotuba yake ya uzinduzi siku ya Alhamisi, Rais Samia amelielezea daraja hilo kuwa ni mradi wa kimageuzi wa miundombinu, akisema linapunguza muda wa kusafiri katika ziwa hilo kutoka saa mbili hadi dakika tano tu.

Ameongeza kuwa daraja hilo pia litasaidia kukuza biashara na nchi jirani.

Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 4.66 limejengwa na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China na Kampuni ya 15 ya Shirika la Reli la China.

Makamu meneja wa mradi huo Qin Rong amesema kuwa asilimia takriban 95 ya wafanyakazi walioshiriki katika ujenzi huo ni Watanzania na kwamba ushiriki wao umeinua kiwango cha ujuzi na kuongeza uzoefu wa wenyeji, utaunga mkono maendeleo ya miundombinu ya nchi hiyo katika siku za baadaye.

Balozi wa China nchini humo, Chen Mingjian amesema Daraja Magufuli ni mradi wa kihistoria chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na mfano wa ushirikiano kati ya China na Tanzania, ukionyesha umuhimu wake kwa maendeleo ya China na Afrika.

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2025 ikionyesha Daraja Magufuli lililojengwa na Kampuni ya China mjini Mwanza, Tanzania. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Picha hii iliyopigwa Juni 19, 2025 ikionyesha Daraja Magufuli lililojengwa na Kampuni ya China mjini Mwanza, Tanzania. (Xinhua/Emmanuel Herman)

Picha iliyopigwa Juni 19, 2025 ikionyesha Daraja Magufuli lililojengwa na Kampuni ya China mjini Mwanza, Tanzania. (Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China/kupitia Xinhua)

Picha iliyopigwa Juni 19, 2025 ikionyesha Daraja Magufuli lililojengwa na Kampuni ya China mjini Mwanza, Tanzania. (Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China/kupitia Xinhua)

Wacheza dansi wakifanya maonyesho kwenye hafla ya uzinduzi wa Daraja Magufuli lililojengwa na Kampuni ya China mjini Mwanza, Tanzania, Juni 19, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha