

Lugha Nyingine
EADB yapata $40M kutoka Mfuko wa OPEC kwa ajili ya kampuni ndogo na za kati na uendelezaji miundombinu
Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imepiga hatua kubwa katika kukuza maendeleo endelevu ya kiuchumi kote Afrika Mashariki kwa kuingia mkataba wa mkopo wa dola milioni 40 na Mfuko wa OPEC wa Maendeleo ya Kimataifa.
Ushirikiano huo unawakilisha mpango mkubwa zaidi wa ufadhili hadi sasa kati ya taasisi hizo mbili.
Makubaliano hayo yamesainiwa kwenye makao makuu ya Mfuko wa OPEC mjini Vienna, na yanalenga kuimarisha kampuni za ukubwa mdogo na wa kati (SMEs) pamoja na miradi muhimu ya miundombinu katika nchi wanachama wa EADB.
Taarifa iliyotolewa na pande hizo mbili inaeleza kuwa, ushirikiano huo ni ishara ya dhamira ya pamoja kati ya EADB na Mfuko wa OPEC katika kukuza ukuaji himilivu na jumuishi katika eneo lote.
Ili kuongeza zaidi athari chanya za ufadhili huo, Mfuko wa OPEC umepewa jukumu la kupanga dola milioni 25 za ziada katika fedha zilizokusanywa, na hivyo kuimarisha uwezo wa EADB kuanzisha mipango mikubwa ya maendeleo.
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma