Uwezo wa China wa kuzalisha umeme waongezeka kwa asilimia 18.8 hadi kufikia mwisho wa Mei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2025

Picha iliyopigwa Desemba 28, 2024 ikionyesha mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo katika eneo la Dabancheng, linalojulikana pia kwa jina la "Bonde la Upepo la China," katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China. (Xinhua/Hu Huhu)

BEIJING – Idara ya Kitaifa ya Nishati ya China imesema jana Jumatatu kuwa, uwezo wa jumla wa China wa kuzalisha umeme umepanda hadi kufikia kilowati bilioni 3.61 kufikia mwishoni mwa mwezi wa Mei mwaka huu, ikimaanisha ongezeko la asilimia 18.8 kuliko ule wa mwaka uliopita.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa, kati ya uwezo wa jumla hiyo, uwezo wa China wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua ulifikia kilowati bilioni 1.08, ukiongezeka kwa asilimia 56.9 kuliko mwaka jana na uwezo wa China wa kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo ulifikia kilowati milioni 570, ni ongezeko la asilimia 23.1 kuliko mwaka uliopita.

Aidha, kwa upande wa uwekezaji, kampuni kubwa za kuzalisha umeme za China ziliwekeza yuan bilioni 257.8 (dola za Kimarekani kama bilioni 35.95) katika miradi ya kuzalisha umeme kati ya Januari na Mei, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.4 kuliko mwaka uliopita.

Mamlaka hiyo imesema kuwa, uwekezaji katika miradi ya gridi ya umeme uliongezeka kwa asilimia 19.8 kufikia yuan bilioni 204.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha