

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu Li wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Singapore Wong
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 23, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amefanya mazungumzo na mwenzake wa Singapore Lawrence Wong, mjini Beijing jana Jumatatu akisema kuwa China na Singapore ni majirani mwema na wenzi muhimu wa ushirikiano na kwamba chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wao, urafiki wa jadi kati yao umekuwa ukizidishwa kila mara tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 35 iliyopita huku uhusiano wa pande mbili ukiimarishwa na ushirikiano wa kivitendo ukipata matunda mengi.
Amesema China inapenda kushirikiana na Singapore kushikilia desturi ya kuheshimiana na kuaminiana, usawa na kunufaishana, wakati huohuo ikidumisha mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu, kuongeza mawasiliano ya kimkakati, na kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa.
Waziri Mkuu Li amesema, China inapenda kutumia kikamilifu utaratibu wake wa ushirikiano wa pande mbili na Singapore, kutekeleza mpango wao wa ushirikiano kwa ajili ya kujenga kwa pamoja Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kupanua na kuimarisha miradi kinara ya ushirikiano.
"China pia inapenda kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji wa pande mbili, kupanua kikamilifu ushirikiano katika masoko ya upande wa tatu, na kuanzisha na kuendeleza mipango mipya ya ushirikiano katika maeneo kama vile uchumi wa kidijitali, uchumi wa kijani, akili bandia, miji mahiri na nishati ya bahari," ameongeza.
Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuimarisha mawasiliano katika elimu, utamaduni, utalii na vyombo vya habari, na kutilia maanani kufungua mlango na ushirikiano wa kweli wa pande nyingi katika kanda hiyo, kuhimiza kikamilifu biashara na uwekezaji kuwa huria zaidi na rahisi zaidi, na kudumisha utulivu na urahisi wa minyororo ya viwanda na usambazaji duniani.
Kwa upande wake Wong amesema kuwa Singapore inatazamia kudumisha mawasiliano na ushirikiano wa karibu wa ngazi ya juu katika nyanja mbalimbali na China, kuzidisha urafiki na hali ya kuaminiana, na kuendeleza miradi kinara ya ushirikiano kama vile Eneo Maalum la Viwanda la Suzhou.
"Pia tunapenda kuchunguza uwezekano wa ushirikiano katika nyanja zinazoibukia kama vile uchumi wa kidijitali, uchumi wa kijani, akili bandia na dawa za kibaiolojia, na kupanua ushirikiano na upande wa tatu na kuboresha mawasiliano ya kiutamaduni" Wong amesema.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Singapore Lawrence Wong, ambaye yuko ziarani rasmi nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 23, 2025. (Xinhua/Liu Bin)
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma