

Lugha Nyingine
Rais Trump atangaza kusimamishwa vita kati ya Israel na Iran
Rais Donald Trump wa Marekani akitembea kuelekea South Lawn kupanda Marine One katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Juni 20, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)
NEW YORK - Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza Jumatatu kwamba Israel na Iran zimefikia makubaliano rasmi ya kusimamisha vita, ikionyesha kile alichokiita mwisho wa "Vita vya Siku 12" ambapo katika ujumbe wake kwenye True Social, Rais Trump ameyapongeza nchi hizo mbili na kusema kwamba usimamishaji huo wa vita ulikuwa uanze takriban saa sita, kufuatia kukamilika kwa operesheni za kijeshi zinazoendelea za kila upande.
Usimamishaji vita wa awali utadumu kwa saa 12, ambapo katika kipindi hicho upande unaopinga utadumisha ishara ya "amani na heshima", ameandika.
Kwa mujibu wa Rais Trump, Iran itaanzisha usimamishaji vita huo, ikifuatiwa na Israel saa 12 baadaye, ikihitimishwa na tangazo rasmi la kumalizika kwa vita hivyo katika muda wa saa 24.
"Kwa kuchukulia kuwa kila kitu kinafanya kazi kama inavyopaswa, ambayo itakuwa hivyo, ninapenda kuzipongeza nchi zote mbili... kwa kuwa na ushupavu, ujasiri, na akili kukomesha kile kinachopaswa kuitwa 'VITA VYA SIKU 12."
Akiyaelezea makubaliano hayo kuwa mafanikio ambayo "yanaweza kuiokoa Mashariki ya Kati kutoka uharibifu wa miaka mingi," Rais Trump amemalizia tangazo lake hilo kwa ujumbe mzito wa umoja: "Mungu ibariki Israel, Mungu ibariki Iran, Mungu ibariki Mashariki ya Kati, Mungu ibariki Marekani, na MUNGU IBARIKI DUNIA!"
Hakujawa na uthibitisho wa mara moja kutoka kwa maafisa wa Israel au Iran. Vyanzo vya habari ndani ya Ikulu ya White House na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon bado havijatoa taarifa rasmi.
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma