Awamu ya pili ya mradi wa kudhibiti kichocho unaoongozwa na China yakamilika Tanzania Zanzibar

(CRI Online) Juni 24, 2025

Utafiti wa awali uliofanywa kwenye eneo la majaribio katika kisiwa cha Unguja, Tanzania Zanzibar, kwa awamu ya pili ya mradi wa msaada wa kiufundi unaoratibiwa na China kuhusu udhibiti wa kichocho umekamilika juzi Jumapili.

Kiongozi wa kundi la mradi huo Dai Yang ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba, tangu mwezi Mei, timu ya mradi huo imekuwa ikifanya utafiti wa kiwango cha maambukizi ya kichocho miongoni mwa wakazi katika jamii tatu za Kinyasini, Kikobweni na Chaani Masingini.

Amesema tathmini iliyofanywa katika maeneo yote matatu imekamilika, huku zaidi ya watu 1,500 wakiwa wamefanyiwa uchunguzi na kiwango cha jumla cha maambukizi kilichorekodiwa kikiwa karibu asilimia 5.

Dai ameongeza kuwa, awamu hiyo ya pili itaendelea kwa utekelezaji wa mkakati jumuishi wa udhibiti katika maeneo ya majaribio kisiwani Unguja, ikiwemo utambuzi wa magonjwa, udhibiti wa konokono, na ujumuishaji wa utaalamu wa Kichina ili kusaidia juhudi za kutokomeza kichocho kisiwani humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha