Guangdong yachukua hatua mbalimbali kuchochea viwanda vya roboti (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2025
Guangdong yachukua hatua mbalimbali kuchochea viwanda vya roboti
Picha hii ikionesha Roboti ya ukaguzi wa bomba kwenye kituo cha uvumbuzi wa roboti cha mkoa mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Juni 25, 2025. (Xinhua/Deng Hua)

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China umekuwa ukichukua hatua mbalimbali ili kuendeleza viwanda vya roboti. Kasi ya kutumia na kuenea roboti za AI imeongezeka katika miji ya mkoa huo ya Guangzhou na Shenzhen, na kituo cha uvumbuzi wa roboti za AI kimeanzishwa mjini Shenzhen.

Aidha, miji kama Foshan, Dongguan na Zhuhai ya mkoa huo inahimizwa kuwezesha kutumika vya kutosha nguvu zao bora za viwanda ili kujenga vituo vya kuzalisha roboti.

Uzalishaji roboti za viwandani wa mkoa huo wa Guangdong ulizidi roboti 240,000 mwaka 2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.2 kuliko mwaka 2023, ukichukua nafasi ya kwanza nchini China kwa miaka mitano mfululizo, takwimu za Idara ya Viwanda na Teknolojia ya Upashanaji Habari ya Mkoa huo wa Guangdong zinaonesha. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha