Kampuni za huduma ya afya za China zatafuta upanuzi katika maonyesho ya tiba ya Cairo (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2025
Kampuni za huduma ya afya za China zatafuta upanuzi katika maonyesho ya tiba ya Cairo
Mtembeleaji maonyesho akizungumza na muonyeshaji kwenye banda la kampuni za dawa na vifaa vya tiba za China katika maonyesho ya nne ya Africa ya Huduma za Afya mjini Cairo, Misri, tarehe 26 Juni 2025. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

CAIRO - Makumi ya kampuni za China za dawa na vifaa vya tiba zinashiriki katika maonyesho ya nne ya Africa ya huduma za Afya mjini Cairo, mji kuu wa Misri yakilenga kupanua uwepo wao nchini Misri na kuingia katika soko linalokua la huduma za afya barani Afrika.

Maonyesho hayo ya siku tatu, yaliyoanza Jumatano na kufungwa leo Ijumaa katika Kituo cha Kimataifa cha Maonyesho cha Misri, yamevutia kampuni takriban 350 za ndani na nje ya Afrika. Miongoni mwao ni angalau kampuni 24 za China zikionyesha bidhaa katika picha za tiba, upimaji na utambuzi magonjwa, dawa, na teknolojia za huduma ya jumla ya afya.

Kwa washiriki wa China, maonyesho hayo yanatoa jukwaa la kuunganishwa na wateja watarajiwa, wasambazaji na maafisa wa serikali.

Waandaaji wa maonyesho hayo wamesema jukwaa hilo linahimiza mawasiliano ya maarifa na ushirikiano ili kuunga mkono maendeleo ya miundombinu ya huduma ya afya kote Afrika.

Maonyesho hayo ni moja ya matukio makubwa zaidi ya biashara ya huduma ya afya katika bara la Afrika, likileta pamoja washikadau kukabiliana na changamoto za pamoja na kutafuta suluhu za siku za baadaye. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha