Mradi wa kusafirisha umeme wa moja kwa moja wa nguvu kubwa ya ±800 kV waanza kazi Ningxia-Hunan, China (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2025
Mradi wa kusafirisha umeme wa moja kwa moja wa nguvu kubwa ya ±800 kV waanza kazi Ningxia-Hunan, China
Picha hii ikionyesha mwonekano wa kituo cha kupozea umeme cha Zhongning, sehemu ya mwisho ya kupeleka umeme ya mradi wa kusafirisha umeme wa nguvu kubwa ya ±800 kV kwa mkondo wa moja kwa moja wa Ningxia-Hunan huko Zhongwei, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, Kaskazini-magharibi mwa China, Juni 29, 2025. (Picha na Yuan Hongyan/Xinhua)

Baada ya majaribio ya saa 168, mradi wa kusafirisha umeme wa nguvu kubwa ya ±800 kV kwa mkondo wa moja kwa moja wa Ningxia-Hunan, umeanza kazi yake rasmi kwa uwezo wa nguvu za kilowati milioni 4 jana Jumapili, ambao unaweza kupeleka umeme kutoka Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wahui wa Ningxia, kaskazini magharibi mwa China hadi Mkoa wa Hunan, katikati mwa China.

Mradi huo wa kupeleka umeme una urefu wa kilomita 1,616 na umepangwa kukamilika kikamilifu na kuanza kutumika kwa uwezo wake uliosanifiwa wa usambazaji umeme wenye nguvu ya kilowati milioni 8 mwezi Septemba mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha