Juhudi za utafutaji na uokoaji zaendelea baada ya mvua kubwa kunyesha katikati mwa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2025
Juhudi za utafutaji na uokoaji zaendelea baada ya mvua kubwa kunyesha katikati mwa China
Waokoaji wakitafuta watu ambao hawajajulikana walipo katika mji mdogo Erlangping wa Wilaya ya Xixia ya Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan, katikati mwa China, Julai 2, 2025. (Xinhua/Hao Yuan)

Mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo ya Taiping na Erlangping ya Mkoa wa Henan, katikati mwa China imesababisha kiwango cha maji ya mto kupanda juu kwa ghafla kwenye sehemu za mitiririko ya maji ya mto katika wilaya ya Xixia juzi Jumatatu, ambapo mafuriko yaliharibu miundombinu na kuacha baadhi ya wakaazi wakiwa wamekwama.

Kufuatia mafuriko hayo, juhudi za uokoaji zilitekelezwa mara moja, huku watu wawili wakiokolewa. Juhudi zaidi za utafutaji na uokoaji zinaendelea katika pilika ya kutafuta watu watatu ambao bado hawajajulikana walipo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha