Kiasi cha shehena kwenye ushoroba kinara wa biashara wa China chaongezeka kwa asilimia 76.9 katika nusu ya kwanza ya mwaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025

Picha iliyopigwa tarehe 3 Julai 2025 ikionyesha kreni zikipakia makontena kwenye treni ya mizigo katika kituo cha kontena cha reli cha Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

NANNING - Kiasi cha shehena kwenye Ushoroba Mpya wa Biashara wa Kimataifa wa Nchi Kavu na Baharini kimeongezeka kwa asilimia 76.9 kuliko mwaka uliopita na kufikia kontena 746,000 za uniti sawa na futi ishirini (TEUs) katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, Kundi la Nanning la Reli ya China limesema, ambapo usafirishaji wa mizigo kwenye ushoroba huo uliweka rekodi mpya kwa kufikia idadi ya kontena 700,000 Juni 20, ikiwa ni siku 125 mapema kuliko ulivyofanya mwaka jana.

Ukiwa ni mradi muhimu chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, ushoroba huo umekuwa ukitekeleza jukumu muhimu katika kuunganisha maeneo ya magharibi ya China yasiyo na bahari na masoko ya kimataifa.

Muundo huo mpya wa usafiri wa aina mbalimbali ulianzishwa Machi 25, wakati treni ya mizigo iliyokuwa imebeba magari 200 kutoka Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China ilipowasili katika Bandari ya Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China ilihamishwa moja kwa moja hadi kwenye meli ya baharini iliyokuwa ikielekea Bandari ya Jebel Ali ya Dubai.

Matumizi haya ya mara ya kwanza ya "treni ya mizigo aina ya JSQ inayochanganya meli ya ro-ro" yalianzisha njia mpya ya usafirishaji kwa magari kutoka mji huo wa Chongqing.

Ushoroba huo pia ulizindua njia unganishi ya usafirishaji bidhaa kwenye reli na bahari mwaka huu, ikipunguza hitaji la wachukuzi mizigo kwa njia ya meli kuratibu kwa nyakati tofauti meli kadhaa zilizobeba mizigo katika sehemu tofauti za usafirishaji, na kuwezesha ufuatiliaji kamili wa shehena ili kuongeza ufanisi na gharama ya chini zaidi.

Kundi hilo la reli limeeleza kuwa, ushoroba huo sasa unafanya kazi kwa njia 14 za treni zisizobadilika ambazo zinaunganisha Bandari ya Ghuba ya Beibu mkoani Guangxi na Bandari ya Zhanjiang katika mkoa jirani wa Guangdong hadi kwenye vituo vikuu vya bara la ndani katika miji ya Chongqing, Chengdu, Guiyang, Lanzhou, Huaihua na Xi'an.

Limeeleza kuwa, bidhaa zinazosafirishwa kupitia ushoroba huo wa biashara kwa njia ya huduma ya kuunganisha usafirishaji kwenye reli na bahari sasa zimehusisha aina 1,236, ikiwa ni 79 zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuhusisha vifaa vya kielektroniki, magari na vipuri vya magari, mashine, vyombo vya umeme nyumbani na vyakula.

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha chombo cha baharini kilichopakiwa makontena kikitia nanga kwenye gati la kontena la kiotomatiki la Bandari ya Qinzhou, katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha mwonekano wa  Bandari ya Qinzhou, katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha mwonekano wa Bandari ya Qinzhou, katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha yadi ya kontena ya gati la kontena la kiotomatiki la Bandari ya Qinzhou, katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha chombo cha baharini kilichopakiwa makontena kikamilifu kikiondoka kwenye Bandari ya Qinzhou, katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha iliyopigwa Julai 3, 2025 ikionyesha chombo cha baharini kilichopakiwa makontena kikiondoka kwenye Bandari ya Qinzhou, katika Mji wa Qinzhou, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha