China kufanya shughuli mbalimbali za kitamaduni kuadhimisha miaka 80 tangu ushindi wa vita dhidi ya uvamizi wa Japan na ufashisti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2025

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China ikifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu shughuli mbalimbali za kitamaduni za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupinga Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 3, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China ikifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu shughuli mbalimbali za kitamaduni za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupinga Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 3, 2025. (Xinhua/Cai Yang)

BEIJING - China itaandaa shughuli mbalimbali za kitamaduni kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupinga Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti ambapo mkutano wa waandishi wa habari umefanywa jana Alhamisi na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China ili kuweka wazi maelezo ya shughuli hizo za kitamaduni, ambazo ni pamoja na tamasha la jioni, maonyesho ya fasihi na kazi zingine za sanaa.

Naibu Waziri wa Utamaduni na Utalii wa China Lu Yingchuan amesema ili kuadhimisha siku hiyo muhimu, wizara hiyo inashirikiana na idara husika kuandaa tamasha na kusimamia uteuzi wa kazi bora za kitamaduni kwa maonyesho.

"Shughuli hizo zinahusu mada za kukumbuka historia, kuheshimu wahanga, kuthamini amani, na kujitahidi kwa mustakabali bora wa siku za baadaye," Lu amesema.

Tamasha la jioni litafanyika Septemba 3 kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing mjini Beijing, na litatangazwa moja kwa moja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG).

"Idadi kubwa ya wasanii bora kutoka kote nchini China wamealikwa, na kizazi kipya cha wafanyakazi wa kitamaduni watachukua jukumu kuu na kushiriki kikamilifu katika shughuli hizo," Lu amesema.

Luo Cunkang, msimamizi wa Jumba la makumbusho ya vita vya watu wa China dhidi ya uvamizi wa Japan amesema, maonyesho husika yatazinduliwa tarehe 7 Julai kwenye Jumba hilo mjini Beijing na yatakuwa na picha 1,525 na vitu vya mabaki 3,237.

Naibu mkurugenzi wa Mamlaka ya Redio na Televisheni ya China Liu Jianguo amesema kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba, maonyesho ya sanaa ya maadhimisho hayo yatafunguliwa kwa umma kwenye Jumba la Sanaa ya Taifa la China ambapo zaidi ya kazi za sanaa 300 zikiwemo picha za jadi za Kichina, picha za mafuta, vitu vilivyochapishwa, sanamu na picha za rangi za maji zitaonyeshwa.

Ameongeza kuwa kuanzia Julai hadi Septemba, kazi bora za sanaa za sauti na video za China zinazohusiana na vita dhidi ya uvamizi wa Wajapan zitatangazwa tena kwenye vituo vya televisheni vya taifa na majukwaa ya mtandaoni.

"Ili kukumbuka historia na kuwaenzi wahanga, filamu karibu 100 kuhusu vita hivyo pia zitaonyeshwa kwenye TV hadi mwisho wa 2025," Wang Xiaozhen, naibu mkuu wa CMG, amesema.

Septemba 3 ni maadhimisho ya Siku ya Ushindi ya vita vya watu wa China dhidi ya uvamizi wa Japan, ili kuadhimisha kutiwa saini kwa Nyaraka za Kujisalimisha kwa Japan Septemba 2, 1945.

Vikiwa vilianza mwaka 1931 na kumaliza mwaka 1945, Vita vya Watu wa China vya Kupinga Uvamizi wa Japan ni vita vya kwanza kuzuka na kampeni iliyochukua muda mrefu zaidi katika Vita vya Dunia dhidi ya Ufashisti. Vita hivyo vilisababisha vifo vya wanajeshi na raia wa China zaidi ya milioni 35. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha