

Lugha Nyingine
Jinsi Chama Kikubwa Zaidi Duniani Kilivyokua
Katika miaka zaidi ya 100 iliyopita, Wafuasi wa Umarx wa China walichagua "kufuata njia ya Warussia" na kuanzisha Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Baada ya safari ya miaka zaidi ya mia moja ambayo ilikabiliwa na changamoto mbalimbali, CPC kimekua kutoka chama kilichokuwa na wanachama zaidi ya 50 mwanzoni mwa kuanzishwa kwake hadi kuwa chama kikubwa zaidi duniani ambacho idadi ya wanachama wake imefikia zaidi ya milioni 100. Safari hiyo tukufu si tu imeshuhudia uhimilivu na hekima ya chama cha CPC, bali pia imeonyesha mvuto wake wa kipekee na uhai wa nguvu yake kubwa.
Katibu Mkuu wa chama hicho Xi Jinping alisema: "Chama cha Kikomunisti cha China ni chama kikubwa zaidi duniani. Kikiwa Chama kikubwa, kinatakiwa kuonesha sura yake ilivyo. Uzoefu wake umethibitisha vya kutosha kuwa, Chama cha Kikomunisti cha China kinaweza kuwaongoza watu katika mapinduzi makubwa ya jamii, na pia kujifanyia mapinduzi makubwa. Lazima siku zote tudumishe nguvu na kuwa na ari kubwa, na daima kuwa watumishi wa umma, watangulizi wa zama, na uti wa mgongo wa taifa." Maneno haya yameelezea wazi kwa nini chama cha CPC kimeweza kuwa chama cha kisiasa kikubwa zaidi duniani.
Chama cha CPC kikiwa chama cha watangulizi wa tabaka la wafanyakazi wa China, na watangulizi wa watu wa China na taifa la China, siku zote kinashikilia nia ya kuutumia umma kwa moyo wote. Kuanzia Mkutano Mkuu wa Pili wa Chama kupitisha "Azimio la Katiba ya Chama cha Kikomunisti", ambalo kidhahiri liliamua kuanzisha "chama kikubwa cha umma", hadi katika zama mpya za kushikamana na wananchi wapatao zaidi ya bilioni 1.4 katika kufanya juhudi za kutimiza lengo kuu la ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawishaji wa taifa, chama cha CPC siku zote kinawaweka wananchi kwenye nafasi ya juu zaidi.
Chama kinasisitiza uongozi wa tabaka la wafanyakazi, lakini kinapinga kuwatetea tu watu wa tabaka la wafanyakazi, kinatilia maanani sana watu kujiunga kifikra na chama hicho, na siku hadi siku kinaimarisha msingi wa kitabaka wa chama, huku kikipanua msingi wa kiumma wa chama.
Ujasiri wa kujifanyia mapinduzi ni tabia wazi ya Chama cha CPC, na pia ni alama wazi inayotofautiana na vyama vingine. Chama kilizaliwa katika hali ya kukumbwa na matatizo ya ndani na nje, kikapita mazingira magumu , na kikakua zaidi katika hali ya kuyashinda mambo mengi yenye taabu kubwa. Kila baada ya kujisahihisha makosa mwanzo wake mpya wa kukua na kupata maendeleo ya chama na mambo ya chama yakaanzia tena.
Ili kudumisha hali yake ya kimaendeleo na usafi wake, chama cha CPC kinashikilia kuachana na yale yaliyopitwa na wakati na yasiyotakiwa na kuingiza mapya, kikivutia nguvu mpya bila kusita, na kuchukua hatua za kioganaizesheni za kufukuza wanachama wasiokidhi matakwa ya chama, na siku zote kinadumisha uhai wa ukuaji wake.
Tangu kuanzishwa kwake, siku zote chama cha CPC kimekuwa kikifuata nia yake ya awali ya kutafuta ustawi wa wananchi wa China na ustawishaji wa taifa la China. Katika vipindi tofauti vya mapinduzi, ujenzi na mageuzi, chama kimekuwa kikionekana kuwa na nguvu ya mvuto, kuwa na nguvu ya kushikamana na watu, kikivutia watu wengi wanaojitahidi kujiendeleza na kukaribia chama na kutaka kujiunga na chama.
Kutoka msanii wa filamu Niu Ben, hadi wahudumu wa afya waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya janga la UVIKO-19, hadi wataalamu na vipaji na watu wa mfano wa kuigwa ambao wameomba kujiunga na chama wakati wa maadhimisho ya miaka 100 ya chama, Chama cha Kikomunisti cha China kinakua na kimekuwa kikubwa zaidi, na uhai wa nguvu yake unaonekana vya kutosha.
Tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha CPC, Kamati Kuu ya Chama imeweka matakwa ya jumla ya "kudhibiti idadi ya jumla ya wanachama, kuboresha muundo, kuinua sifa, na kutoa mchango," na imeweka mkazo zaidi katika kuhimiza chama kikubwa kukua zaidi kuwa chama chenye nguvu.
Wakati wa kuandikisha wanachama wapya, chama kinadhibiti vikali uingiaji na kufuata kwanza vigezo vya kisiasa; katika utoaji mafunzo kwa wanachama, kinafuatilia zaidi mafunzo mazuri na yenye ufanisi kwa kutumia Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya kuunganisha mioyo na nafsi; katika usimamizi wa wanachama, kusisitiza zaidi mafunzo muhimu na yenye ufanisi; na kuchukua hatua sahihi na zenye ufanisi katika utoaji wa mafunzo na kufanya usimamizi, na katika kufuata nidhamu kali, kuhakikisha hali ya kimaendeleo ya chama, na usafi wake, na kuweka ujenzi wa nidhamu ya chama kwenye nafasi muhimu zaidi.
Kila mwanachama ni bendera moja. Katika mstari wa mbele wa mageuzi na maendeleo, wanachama wanatekeleza ipasavyo majukumu yao na kufanya uvumbuzi katika nafasi zao za utendaji; katika uwanja mkuu wa kuwasaidia watu wenye umaskini kujiendeleza na kuondokana na umaskini, wanachama zaidi ya milioni 3 wamefanya juhudi kubwa kwenye mstari wa mbele, na wanachama zaidi ya 1,800 wa CPC walijitolea mihanga kwenye mstari wa mbele; katika mapambano dhidi ya janga la UVIKO-19, wanachama zaidi ya milioni 7 walikwenda mstari wa mbele kulinda maisha na afya ya watu, na maafikiano na utulivu wa jamii. Wanachama wengi zaidi wanatangulia kufanya juhudi katika kusukuma mbele maendeleo ya sifa bora, kuboresha usimamizi wa mashinani, na kutekeleza kazi za dharura, ngumu na hatari, na kuwa nguzo kuu ya kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya chama na nchi.
(Mwandishi ni naibu mkurugenzi na profesa wa ofisi ya Mafunzo na Utafiti wa Ujenzi wa Chama katika Chuo cha Kamati Kuu ya Chama (Chuo cha Mambo ya Utawala cha Kitaifa). Makala hii imefupishwa kwa kiasi fulani.)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma