Waziri Mkuu wa China atoa wito kwa nchi za BRICS kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mageuzi ya usimamizi wa dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 07, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumapili wakati akihutubia kikao cha wajumbe wote cha "Amani na Usalama na Mageuzi ya Usimamizi wa Dunia" cha Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihutubia kikao cha wajumbe wote cha "Amani na Usalama na Mageuzi ya Usimamizi wa Dunia" cha Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS  jana Jumapili huko Rio de Janeiro, Brazil. (Xinhua/Liu Bin)

RIO DE JANEIRO - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumapili wakati akihutubia kikao cha wajumbe wote cha "Amani na Usalama na Mageuzi ya Usimamizi wa Dunia" cha Mkutano wa 17 wa Kilele wa BRICS amesema kuwa nchi za BRICS zinapaswa kujitahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mageuzi ya usimamizi wa dunia, akitoa wito kwa chombo hicho kulinda amani na utulivu duniani.

Viongozi wa nchi za BRICS walihudhuria mkutano huo ulioongozwa na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil.

Li amesema kwa sasa, mabadiliko ambayo hayakuonekana katika miaka 100 iliyopita yanajitokeza kwa kasi kubwa, sheria na utaratibu wa kimataifa vinakabiliwa na changamoto kubwa, na mamlaka na ufanisi wa taasisi za pande nyingi unaendelea kupungua.

"Maono ya usimamizi wa dunia yaliyotolewa na Rais Xi Jinping wa China, yenye umaalum wa mashauriano ya kina, mchango wa pamoja na kunufaisha manufaa, yamekuwa yakionyesha thamani yake ya kisasa na umuhimu wa kivitendo," Li amesema.

Amesema, katika kukabiliana na kuongezeka kwa migogoro na tofauti, inahitajika kuimarisha mashauriano ya kina kwa msingi wa usawa na kuheshimiana; katika kukabiliana na maslahi ya pamoja yanayoingiliana kwa kina, inahitajika kutafuta mchango wa pamoja kupitia mshikamano; katika kukabiliana na fursa za maendeleo zenye manufaa kwa pande zote, inahitajika kuwa na mawazo wazi ili kutafuta kufanikishana na kunufaishana manufaa.

"Kama nguvu ongozi ya kundi la Nchi za Kusini, nchi za BRICS zinapaswa kushikilia uhuru na kujitegemea, kuonyesha uwajibikaji wao, na kuchukua jukumu kubwa zaidi katika kujenga maafikiano na kuuwiana," Li amesema.

Waziri Mkuu huyo wa China ametoa wito kwa kundi hilo kushikilia kwa dhati maadili na haki, na kutafuta suluhu za kimsingi kwa msingi wa hali halisi ya kila suala.

Akisema kuwa China itaanzisha kituo cha utafiti cha China na BRICS kuhusu nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora mwaka huu, Li pia ametangaza ufadhili wa masomo ulioanzishwa kwa ajili ya nchi za BRICS ili kuwezesha ukuzaji vipaji katika sekta zikiwemo za viwanda na mawasiliano ya simu.

Mkutano huo umepitisha Azimio la Rio de Janeiro la Mkutano wa Kilele wa 17 wa BRICS.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha